Kwa mwanaume hakuna kitu kigumu kama hiki, kuna ambao hugundua kuwa wana matatizo ya nguvu za kiume tangu wakiwa wadogo na kuamua kutokutafuta wanwake kabisa. Lakini kwa sasa kuna wengi ambao hugundua kuwa wana matatizo haya wakati wakiwa kwenye mahusiano au baada ya ndoa. Najua kama una hili tatizo ushahangaika sana na dawa, kuna wanaopona na ambao hawaponi, kuna ambao zinaisha kabisa na wengine huwa nazo kidogo. Najua ni ngumu kuishi na hili tatizo hivyo mbinu zifuatazo zitakusaidia sana kuishi kwa amani katika ndoa yako.
(1) Sio mwisho wa ndoa yako/Mwanamke anaweza kukuvumilia; Utaanza kwa kujidharau, kudhani labda mke wako taakuacha, kudhani labda atakudharau na kudhani labda ndiyo mwisho wa ndoa yako. Labda nikuambie kitu si mwisho wa ndoa yako, wanawake si warahisi kutoka kwenye ndoa namna hiyo na niwavumilivu mpaka basi. Acha kupaniki, acha kujidharau, mke wako hakudharau na kama ukiwa muwazi yupo tayari kukusaidia na kama ukijiamini hata unaweza kufurahia tendo la ndoa na nguvu hizo kidogo.
Wanawake wengi hata hawajui kama wanaume wao wana hili tatizo, huanza kujua baada ya wewe mwanaume kubadilika na kuwa na kisirani. Hapo ndipo huanza kuuliza kwa mashoga zake, kutafuta ushauri kwa makungwi na watu kama mimi ndipo anaambiwa ukweli. Ukiacha kupaniki, ukamheshimu mke wako, ukasingizia labda uchovu au ukabadilisha vyakula mke wako akawa na amani ndani ya ndoa nina uhakika atakuvumilia, hatataka kukutangaza kwakua hatataka kukuacha, manyanyaso ndiyo yatamlazimisha kutafuta msaada nnje na si upendo hivyo acha kupaniki.
0 Maoni