
wako baba /kaka
Kama kweli unampenda mpenzi wako, basi jaribu sana kuepuka sifa za kijinga.
Kuna baadhi ya mambo ya kijinga unayafanya, ila kwavile unaona anakuvumilia, anakulilia, anakunyenyekea, anaomba msamaha hata kama kosa sio lake.
Basi una vimba bichwa, unajiona wewe ndo wewe, unamuendesha unavyotaka.
Wake up, uvumilivu una mwisho wake, ipo siku atachoka ujinga unaomfanyia.
Atakutoa moyoni, na kuamua kumove on.
Tatizo litabaki kwako, utalia na kusaga meno, utahangaika usiku kucha kutaka kumrudisha lakini haitawezekana.
Kwake utabaki story tu.
Be smart, usimkerahishe mpenzi wako kwa makusudi.
Mpe furaha na kulijenga tabasamu lake kila kukicha.🚶🏾♂🚶🏾♂🚶🏾♂🚶🏾♂badilika acha mapenzi na maisha ya mazoea mambo yamebadilika..... Kuna baadhi ya tabia za wanawake, hutakiwi kuzichukulia hasira wala kumletea ubabe ubabe.
Inahitajika akili ili uweze kwenda nazo sawa.
Unaweza fanya jambo dogo tu, utashangaa mwanamke wako kakununia, au hata kujifanya kakasirika, au kususa kabisa.
Kwa mwanaume mjinga, anaweza jikuta anamtukana mwanamke wake au hata kumpiga makofi.
Lakini kwa mwanaume mwerevu anajua kuwa mwanamke anahitaji kulelewa kama mtoto, anahitaji kubembelezwa.
Badala ya kumtusi au kumpiga, anaamua kumsogelea karibu na kumbembeleza kimahaba na utashangaa anamwagika na kutoa ya rohoni mpaka ushangae...... Haihitaji nguvu nyingi kuishi na mwanamke, inahitaji akili tu ya kujua ufanye nini ili uende nae sawa, ufanye nini ili umteke kihisia ili ufurahie mapenzi yenu.🚶🏾♂🚶🏾♂🚶🏾♂🚶🏾♂ Unahitaji mtu atakaye kupenda kwa jinsi ulivyo.
Huna kipato kikubwa, huna nyumba, huna gari, kuwa mkweli, wala sio tatizo.
Tatizo ni pale utakapotaka kuigiza, au kuyaishi maisha ambayo si yako ili tu upendwe na yule umpendae.🚶🏾♂🚶🏾♂🚶🏾♂badilika kijana acha kuwa mpumbavu akikosa hayo mavituz uliyonadi kumiliki halafu akavikosa unadhani atabaki kwako?
Au hujui mapenzi ya kweli bila kutanguliza pesa bado yapo?
Waliofuata mapenzi ya dhati ni kina mama zetu ambao ndio kizazi cha mwisho lakini sasa ni mabusiness na mabisahara kuwa mkweli akupende wewe jinsi ulivyo ili mkatengeneze paradiso yenu,usimvute kwa kitu utachukia mapenzi maisha yako yote....
0 Maoni