MAMBO NANE 8 YANAYODHOOFISHA NDOA KWA HARAKA.

Related image

1. Utovu wa Adabu: kutamka mambo mabaya au yenye kuchukiza, utani ulioptiliza na kutukanana.
2. Kupuuza: Kutojibu salamu au kutomsikiliza vizuri mwenzako.
3. Urongo na kudanganyana. Hii ni miongoni mwa sumu mbaya sana zinazoweza kuangamiza ndoa kwa haraka.
4. Kuvunja ahadi na kutotunza amana unapoaminiwa.
5. Kumkwepa mwanzako: Ukiwa mtaani unawakumbatia marafiki zako, lakini kwa nini ushindwe kumpa kumbatio hata kidogo mkeo?
6. Dhana mbaya na kusengenya. Ukiifanya dhana na hisia kuwa msingi wa maisha yako utakonda sana. Ishi kwa uhalisia, usiishi kwa hisia.
7. Kushughulika kupita kiasi: Tenga muda kwa ajili ya mwenza wako. Mkipeana muda wa kusikilizana na kufurahishana itaimarisha taasisi yenu ya ndoa na familia.
8. Kutokuwa karibu na Muumba wenu na kuacha kumuabudu. Hili linaweza kusababisha matatizo makubwa katika familia na kuzifanya zisambaratike haraka sana.

Chapisha Maoni

0 Maoni