
1. Ishi kama mwanamke... vaa uhusika wote wa kike.
2. Vaa vizuri na uvutie. Kama ni mama wa nyumbani, usikae na nguo za kulalia kutwa nzima. Hakikisha unavutia mbele ya mumeo.
3. Nukia vyema.
4. Usiyabwage matatizo yako kwa mumeo pindi anapoingia nyumbani. Mpe muda kidogo wa kupumzisha akili yake.
5. Epuka kuendelea kumuuliza "UNAWAZA NINI?" Kwa sababu mawazo ya mwanaume yako random kama matokeo ya google search, ni tofauti na mwanamke. Wanawake mawazo yao yanakuwa organized kama mafaili yaliyopangwa vizuri kabatini.
6. Epuka kuwa mama lawama usiyeishi kulalama kwa kila jambo na kuwa msumbufu.
7. Epuka kabisa kumwambia yeyote matatizo ya ndoa yako kwa kisingizio cha kutaka msaada, hata kama wewe ndiye uliyetendewa mabaya. Kama unahisi kuwa kweli unataka kutatua matatizo ya ndoq yako, basi mtafute mtu sahihi.
8. Jitahidi kuwa mwema kwa mama mkwe, kama ambavyo ungependa mumeo awe mwema kwa mama yako.
9. Jifunze haki na wajibu katika ndoa, usiangalie tu haki zako, bali tazama pia wajibu wako.
10. Mumeo anapokuja nyumbani kimbilia mlangoni, kana kwamba kwamba ulikuwa ukimsubiri kwa shauku. Tabasamu na umkumbatie.
11. Dumisha usafi wa nyumba yako, angalau kwa kiwango anachokitaka.
12. Msifu kwa vile vitu ambavyo unajua hajiamini, kama vile muonekano, akili na kadhalika. Hilo litampandishia morali na heshima.
13. Mwambi kuwa yeye ni mume bora kabisa.
14. Watembelee ndugu zake mara kwa mara au kuwasiliana nao.
15. Anapofanya kazi fulani nyumbani, mshukuru. Hiyo itamhamasisha kufanya zaidi.
16. Anapozungumzia jambo ambalo halina msisimko, msikilize huku ukitikisa kichwa. Uliza hata maswali ili kufanya ionekana kwamba umevutiwa na anachokizungumzia.
17. Mhamasishe kufanya mambo mema.
18. Kama ana mood mbaya, mpe fursa na nafasi ya kutulia. Hali hiyo itaondoka tu.
19. Mshukuru kwa dhati kabisa kwa juhudi yake ya kukuhudumia na utafutaji wa riziki. Ni jambo muhimu sana.
20. Kama amekukasirikia na akaanza kufoka, muache afoke huku wewe ukiwa kimya. Utaona ugomvi wenu unakwisha haraka sana. Kisha akitulia, unaweza kumweleza mawazo yako na namna unavyopenda abadilishe jambo fulani.
21. Unapomkasirikia, usimwambia "unanichefua", badala yake sema "kitendo hiki kinanisikitisha". Elekeza hasira yako kwenye kitendo, badala ya kuielekeza kwake moja kwa moja.
22. Kumbuka kuwa mumeo ana hisia, hivyo ziheshimu.
23. Muache afurahie na marafiki bila kumfanya ahisi kuwa ana hatia, hususan kama marafiki hao ni watu wazuri. Mhamasishe kwenda nje, asiwe mtu wa kukaa nyumbani tu.
24. Kama mumeo ameudhika kwa jambo dogo na wewe unaweza kuliacha, basi liache.
25. Jifunze namna ya kumwambia unachokitaka kwake bila kumfanya aanze kubahatisha. Jifunze namna ya kuwasilisha hisia zako.
26. Usichefuke kwa vitu vidogo. Hisia zako zina thamani kuliko vitu hivyo.
27. Tengeneza utani. Kama maumbile yako sio ya utani, waweza kujifunza namna ya kulifanya hilo, hata mtandaoni.
28. Mwambie na umuoneshe kuwa wewe ni mke bora, na jisifu kwa baadhi ya mambo ambayo unajua kwamba unayamudu vizuri sana.
29. Mpikie chakula bora anachokipenda, sio bora chakula. Hakika njia ya kuingia moyoni mwa mwanaume ni kupitia tumbo lake.
30. Kamwe usimzungumzie vibaya kwa marafiki na wanandugu.
31. Tumia muda wako vizuri na hakikisha umeyakamilisha mambo yako kwa wakati. Tumia muda wako kujifunza vitu vyenye faida, badala ya umbea.
32. Wewe ni kama vazi kwa mumeo, na yeye ni kama vazi kwako; usiyaoneshe mapungufu ya mumeo, na msaidie kuyashughulikia kwa busara.
33. Mwambie mumeo kuwa wampenda... Mwambie hivyo mara nyingi.
34. Itunze afya yako; usibweteke ukauachia mwili wako. Hakikisha unakuwa mama imara, mke imara, mjenzi imara wa nyumba.
35. Jipambe kwa adabu njema. Usinyanyue sana sauti yako unapocheka unapoongea na hata unapotembea.
36. Usiondoke nyumbani bila ruhusa yake, na bila yeye kujua.
37. Hakikisha mavazi yake yote yako safi na nadhifu muda wote.
38. Katika sala na maombi yako ya kila siku, muombe sana Mungu aimarishe na kuyalinda mafungamano ya upendo na huruma kati yenu. Hakika siku zote Shetani atajitahidi kutengeneza migogoro na ugomvi kati ya wanandoa ili waachane.
39. Mtegee sikio anapoongea. Usimkatishe na kuchomekea mambo yako.
40. Jitahidi usiwe na matumizi yasiyo na ulazima au yasiyoendana na kipato cha mumeo.
41. Jifunze mbinu za kumridhisha mumeo kitandani. Kwani hitajio nambari la mwanaume ni tendo la ndoa.
42. Andaa USIKU WA MUME. Hapo ni wewe na yeye tu. Zingatia njia tulizofundisha darasani kuhusu maandalizi ya USIKU WA MUME ambayo hayahusishi watoto kabisa.
43. Kama huridhiki naye kitandani, ongea naye vizuri na umsaidie pia katika kushughulikia jambo hilo. Usisubiri mambo yakawa mabaya kabisa.
44. Kumbuka kuwa kitu cha kwanza ambacho mwanaume anakitazama kwako anapokutana na wewe ni LIPS zako. Hakikisha zina mvuto kwa ajili yake.
45. Kamwe usizungumze naye mambo nyeti au yenye utata akiwa amechoka au akiwa anahisi usingizi. Tafuta muda sahihi wa kuongea naye.
46. Jifunze kushuka. Epuka kujimwambafai.
47. Endelea kufanya mambo mazuri kwa ajili ya mumeo, usipuuze.
48. Kumheshimu na kumtii ndio msingi... Hilo ndio hitajio lake la kwanza kama mwanaume na kama mume. Mengine yote hayatakuwa na maana yoyote ukishindwa hili.
49. Usimlinganishe mumeo na mwanaume yeyote yule, na usiilinganishe ndoa yako na ndoa yoyote ile.
50. Yafanye maisha ya ndoa yako kuwa mali yako binafsi, sio mali ya umma. Uliolewa na mumeo, hukuolewa na Facebook, Instagram au WhatsApp.
Nakumbea kwa Mungu aimarisha mahabba yenu.
0 Maoni