Mwanaume mmoja alimuoa msichana mrembo sana. Yule mwanaume alimpenda sana mkewe. Basi siku moja Yule mkewe kapata gonjwa la ngozi, Taratibu Yule mwanamke akaanza kupoteza ule urembo wake. Tukio hilo limetokea wakati mumewe akiwa safarini, mwanaume aliopata taarifa juu ya tatizo la mkewe. Baadae wakati mwanaume anarudi katika safari yake, nae akapata ajali na kusababisha kupoteza uwezo wake wa kuona (Alipata upofu)
Ingawa maisha yao ya ndoa yaliendelea vizuri bila kuonekana shida yoyote lakini siku zilivyozidi kwenda Yule mwanamke akazidi kupoteza ule urembo wake kutokana na ule ugonjwa wa ngozi. Mumewe kwakua ni kipofu hakujua hilo na hakukua na totfauti yoyote katika yao ya ndoa, Mwanaume aliendelea kumpenda mkewe na mwanamke alimpenda sana mumewe.
Maisha yao yaliendelea kuwa yenye furaha, wakapendana sana, Basi katika hali isiyokua ya kawaida Yule mwanamke akafa! Kifo cha mkewe kilimpelekea mwanaume kuingia katika shida, mawazo kibao na kuwa mwenye huzuni sana. Shughuli za mazishi ziliisha vizuri na akataka aondoke katika ule mji.
Jamaa mmoja alikua nyuma yake alimuita na kumuliza “SASAIVI UTAWEZAJE KUTMBEA PEKE YAKO? SIKU ZOTE MKEO ALITUMIKA KAMA MSAADA WAKO” Yule mwanaume alijibu “MIMI SIO KIPOFU, NILIKUA NAIGIZA TU KWASABABUKAMA MKE WANGU ANAGEJUA KUWA NINGEWEZA KUONA HALI YA NGOZI YAKE KUTOKANA NA UGONJWA , INGEMUUMIZA ZAIDI YA UGONJWA WENYEWE. MIMI SIKUMPENDA MKE WANGU KUTOKANA NA UREMBO WAKE PEKEE, BALI NILIMPENDA ILI NIMJALI JINSI ALIVYO, NILIMPENDA KWA MAPENZI NA UPENDO NDANI YA MOYO, HIVYO NILIGIZA UPOFU. KITU PEKEE NILICHOKUA NAKITAKA NI KUMFANYA AENDELEE KUWA MWENYE FURAHA”
>TUJIFUNZE UNAPOMUOA MWANAMKE KWASABABU YA SURA YAKE JUA SURA INAWEZA KUPOTEA, UNAPOMPENDA KWASABABU YA MAKALIO YAKE HATA HAYO YANAPOTEAGA, UNAMPOMPENDA KWASABABU YA MAZIWA YALIYOSIMAMA KUMBUKA IPO SIKU YATALALA, WALE WAKUANGALIA MWENDE WAKE, UMBO, MACHO YA DUARA HIVYO VYOTE VINAPOTEAGA. HAKUNA MWENYE AHADI NA MUNGU. JIFUNZE KUPENDA KWA DHATI.
DADA UNAMPENDA MWANUME KWASABABU ANA SIX PARK, HANDSAME, ANAPESA NA VITU KAMA HIVYO JUA VINAWEZA KUTOWEKA PENDA PALE MOYO WAKO ULIPOPENDA, JARIBU KUFIKIRIA SIKU HIVYO ULIVYOMPENDEA VIKITOWEKA.
0 Maoni