
Wanawake wanachepuka, tena ukiangalia unaweza kukuta wake watu wanachepuka zaidi kuliko waume za watu. Naongea nao kila siku lakini pamoja na kuchepuka kwao wao ndiyo wanaongoza kwa visirani. Wanawane wengi mume anapokua Malaya, mwanaume anapokua anamnyanyasa huamua kuenda kutuliza akili yake kwa kutafuta mwanaume mwingine na kuchepuka, wengi hutafta waume za watu, wanakua nakaamani ka muda mfupi lakini hawawi na furaha!
Sanasana kikubwa wanachopata ni utamu wa tendo la ndoa na kule kujaliwa lakini kwenye nafsi zao wanakua bado wana visirani, hawana amani. Hii ni kwasababu kuwa furaha yao inawategemea wanaume, kwamba alikua ananyanyaswa na mume wake hana amani badala ya kutafuta amani ndani ya nafsi yake anaenda kutafuta amani kwa mwanaume mwingine.
Atafurahia kidogo lakini kama yule mwanuame naye akianza kumzingia au mke akigundua wakaanza kugombana anarudi kulekule kwenye mawazo na visirani. Sikupangii maisha yako lakini usichepuke kwakua huna furaha bali chepuka kwakua umeamua, sijui kama mmenielewa lakini, nilichoka kusema nikuwa, kama unachepuka kwakua mume wako anachepuka huna raha basi hata kuchepuka kwenyewe hutakufurahia au utakufurahia kwa muda kisha baadaye unarudia kisirani chako.
Nilazima furaha yako isimtegemee mwanaume, iwe yako mwanaume awe kama tu soda kwamba ukisikia kiu unakunywa lakini usipoipata bado unaraha na maji yako, ila ukimfanya mwanaume kama chakula kwamba asipokufurahisha wewe huna raha basi utakua ni mtu wa kubadilisha wanaume kila siku na hutakua na furaha. Fanyia kazi sehemu ya Nne ya kitabu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” usisome tu, hapana, soma na fanyia kazi.
0 Maoni