KUNA KABINTI KADOGO KAKO NDANI YAKE KADEKEZE!

Kuna kabinti kadogo kako ndani yake, haijalishi umri wake, haijalishi amepitia mengi kiasi gani, haijalishi ni mpiganaji kiasi gani, haijalishi kazi anayofanya na wala haijalishi ujanja wake.
Kila mwanamke ana kabinti kadogo sana kapo ndani yake, kabinti ka miaka miwili ambako kanahitaji kudekezwa, kununuliwa zawadi, kusikilizwa na kujaliwa.
Kanahitaji kulia na kubembelezwa, kulalamika na kusikilizwa. Ni kazi yako wewe mwanaume kuhakikisha unakatoa hako kabinti na kukadekeza kweli, kuhakikisha unapokuwa na mkeo kuna muda wa kuwa na hako kabinti na muda mwingine wakuwa na mkeo.
Ndiyo mwanamke hatakiwi kukua moja kwa moja, ili awe mwanamke nilazima uweze kumruhusu kuwa binti hapa na pale, kuna mambo mengine atayafanya utayaona ya kitoto.
Utamshangaa kwa umri wake bado anataka icecream, anataka kubebwa, analilia zawadi, anaogopa mende, analialia akikasirishwa, usishangae, jua ni hako kabinti kanatoka.
Karuhusu katoke kwani ndiyo raha yenyewe ya mapenzi. Usitake mkeo kuwa Gentleman, eti hutaki awe na mambo ya kike, sasa kwanini ulioa mwanamke kama unataka mtu wenye mambo ya kiume?

Chapisha Maoni

0 Maoni