JINSI NILIVYOMFUMANIA MUME WANGU NA MWANAUME MWINGINE!

Habari Kaka Iddi, naomba ficha jina langu sema naomba nipostie kisa changu kwani wanaume ni nyoko. Nimeolewa ndoa ya kanisani kabisa mwaka wa kumi sasa na ndoa yetu ni zile ambazo kila mtu anazitamani.
Sasa Kaka mara zote mimi nimekua nikijisifia mume wangu hivi mume wangu vile kwani ananihudumia kwa kila kitu na ananijali sana. Ni wale wanaume ambao anaweza hata kukumbatia mbele za watu, kwangu alinijali na niliona ndiyo mapenzi.
Basi Kaka mume wangu simu yake niko huru nayo, na ya kwangu yupo huru nayo, katika kipindi chote hicho hakuwahi kunionyesha hata dalili za kwamba anachepuka. Tena akiona wanawake wengine wala hata hageuki hata kama ni mzuri vipi kitu ambacho kilinipa amani.
Sasa Kakab kama wiki mbili zilizopita, alikuja rafiki yake mmoja. Nirafiki wa muda mrefu ambaye mara nyingi anakuja pale nyumbani, yeye anaishi Mwanza, nimfanyabishara hivyo wakati akija Dar hushukia kwetu kwakua nyumba ni kubwa na ni mtu mstaarabu, tena akija analeta mizawadi, mara samaki ambao tunaweza hata tutumie wiki basi natamani aje tu.
Niwale wageni ambao hawachoshi, kwamba akija hata watoto wanafurahia Anko kaja kwani vihelahela na hata shopping inafanya. Sasa basi si ndiyo akaja nyumbani. Kama kawaida kaja na zawadi zake nyingi, tukampokea ndiyo hivyo mambo yakawa moto.
Mara nyingi akiwepo usiku hua wanatoka na mume wangu, mume wangu si mnywaji sana ila huyo ndiyo rafiki yake mkubwa hivyo wanatoka wote, hiyo hata mimi inanipa amani kwani mume hachepuki hivyo hata wakichelewa sana sijali na huwa hata wakichelewa hawarudi wakiwa wamelewa sana.
Sasa safari hii walipotoka mume wangu alirudi peke yake, ilikua ni usiku hivyo sikumuuliza sana nikajua labda shemeji kapata mtu na ingawa kaoa lakini sikutaka kumfuatilia. Lakini nilihisi kitu, mume wangu hakuwa na furaha kabisa, alikua na mawazo na alionyesha ni kama alikua analia, nilimuuliza nini tatizo akasema hajisikikii vizuri.
Ilikua kama saa nane usiku na kwakua walishakula basi tulipanda kitandani, hakutaka hata kuingia bafuni kuoga. Sasa usiku sijui kwanini lakini sikupitiwa na usingizi kabisa, lakini na mume wangu hakulala, muda wote niliona mwanga wasimu, alikua anapiga simu lakini anaambiwa simu haipatikani.
Yaani anapiga tena baada ya dakika kumi na jibu linakua hilohilo, nikajigeuza na kuanza kuchungulia, hapo naona anandika meseji na kutuma, yaani alikua kama kachanganyikiwa. Nilitaka kunyanyuka kumuuliza tatizo nini lakini nilijua kua nitaharibu mambo.
Asubuhi ndipo alipitiwa na usingizi, nilivizia na kuangalia simu yake alifuta sms zote na hata watu aliokua anawapigia. Niliamua kukaa kimya, ilikua ni Jumapili hivyo niliwaandaa watoto kwenda kanisani, yeye alisema hajisikii vizuri hivyo hawezi kwenda.
Nilishangaa sana kwani ndiyo ilikua mara yake ya kwanza tangu tuoane kusema kuacha kwenda kanisani, haijawahi tokea. Lakini niliamua kumpa nafasi na kumuacha. Nilienda kanisani na mchana baada ya misa nilirejea nyumbani.
Watoto niliwapeleka kwa mdogo wangu ambaye alikua anawapeleka beach hivyo nilirejea nyumbani peke yangu. sikurudi na gari nililiacha huko huko kwa mdogo wangu kwaajili ya kuwapelekea watoto beach kwani yeye hana usafiri nikachukua Bajaji kwani si mbali na kuenda nyumbani.
Kufika geti dogo lilikua wazi tena ile wazi kabisa, nilishangaa kwani hua tunafunga, niliingia nakwenda moja kwa moja mlangoni. Ile naaka kufungua tu mlango nikasikia kelele, nisauti ambazo nilikua nazifahamu, mume wangu na shemeji yangu.
“Nisamehe mpenzi nisamehe, sikufanya makusudi na yule si mtu wangu, yule kaka nimezoeana naye tu na wala sijawahi kuafanya naye chochote” mume wa wangu alikua analalamika, nilistuka nikaenda dirishani kuchungulia, nilimkuta mume wangu kapiga magoti analia kama mtoto mdogo.
Shemeji yangu hataki kumsikiliza anataka kuondoka huku akisema kuwa yeye kaenda pale kuchukua nguo zake tu na vitu vyake lakini mapenzi basi. Nguvu ziliniishia mume wangu alikua analia kama mtoto, alivua shati na suruali akabaki na boxer akamrukia na kutaka kumkumbatia shemeji.
Shemeji alimsukuma lakini alimzidi nguvu, mume wangu alimuanguasha kwenye kochi na kuanza kumbusu mdomoni na kila sehemu. Nikama shemu mahaba yalimzidi akatulia, niliona ujinga sikuweza kuvumilia, nilisukuma mlango ambao ulikua umeegeshewa tu.
Wote walistuka kuniona, walipigwa na butwaa nilianza kutukana na kuogea kwa hasira, shemeji alikimbia na kunipiga kikumbo akaondoka, akatoka akikmbia. Yaaai huwezi amini mume wangu ainiahca pale na kuaanza kumkimbiza huku akimuambia nisubiri, usikimbie hatujayamaliza.
Shemeji hakurudi mume wangu alirudi kakasirika, nilijaribu kumuongelesha lakini hakujali, aliingia chumbani na kukaa kama dakika tano kisha akatoka kavaa kabisa anataka kutoka. Nilikua bado nimechanganyikiwa alikuja na kuniamba kuwa anatoka na anamfuata shemeji, nilikasirika na kumuambia kwanini ananifanyia hivyo.
Akaniambia tena akijibu kwa kujiamini bila aibu kuwa yule ni mpenzi wake tangu wakiwa “O” level, akasema yeye ni shoga na hawezi kuacha wala kua na mwanaume mwingine kwani ni aibu. Bila kuonyesha kujuta aliniambia nimvumilie tu.
Unajua kaka nilishangaa kwani hakuonekana kujuta, alikua anongea kama kitu cha kawiada,. Nilimuambia siwezi kukaa pale naondoka aliniambia kwani nakosa nini pale, akaniambia kama naondoka niondoke lakini nitajua mwenyewe chakuwaambia watoto kwani yeye hajali, kama ni aibu basi ni aibu yetu wote na watoto.
Aliondoka na kuniacha nina mawazo, ni wiki sasa Kaka nakuandikia sijui nifanye nini? Mume wangu hata hajali ananafanya kama vile hakuna kilichotokea na kila nikitaka kusema ananiuliza kwani sikuhudumii, kwani si kuridhishi kitandani shida yangu nini?
Hapa nipo njia panda nawaza niondoke au la maana mume wangu kubadilika habadiliki. Hata nikita ndugu itakua ni aibu tu kuwaambia kuwa mume wangu nishoga na bahati mbaya yeye wlaa hajali anasema ni maisha yake na atajuana yeye na Mungu wake! ushauri wenu jamani?
**MWISHO

Chapisha Maoni

0 Maoni