Kama una mchumba wako ni mlevi, Malaya na umekubali kuolewa naye unatakiwa kujua kua hawezi kubadilika, hivyo ukikubali kuvaa Shela hembu jiandae na kuvumilia, sio unaingia kwenye ndoa siku mbili unaanza kusumbua ndugu zako eti mwanaume halali nyumbani, mara katembea na mdogo wangu, oooh nimemfumania na rafiki yangu, mwanaume katembea na rafiki zako wote na umemfumania na bado anakuambia anakupenda na wewe unajichekelea!
Hivi dada zangu mna akili za namna gani? Uko na mwanaume eti kila siku anchat na X wake tena mbele yako anakuambia ni rafiki tu eti na wewe unakubali! Hivi mnakua mnawaza nini, ni kwamba mnaamua kujifanya wajinga au ni wajinga kweli? Hivi mwanaume katembea na mdogo wako wa damu halafu unakubali akuoe eti kisa kakuambia amejifunza amebadilika! Kashatembea na mabaa medi wote mtaanui na kila siku unakuta chupi mpya kwake na bado anakuambia nataka nikuoe!
Mwanaume hujawahi kumpigia simu usiku akakuambia yuko nyumbani, kila siku yuko Baa ni mlevi mbwa lakini bado anakuambia nitaacha kunywa pombe na wewe unakubali! Hivi mnafikiri pombe ni kama Malimau au Pilipili kwamba mtu unaweza kusema naacha leo na kesho ukaacha! Mnaboa sana Dada zangu, unaingia kwenye ndoa ukijua kabisa jamaa ni sifuri lakini baada ya mwezi tu unaanza kumsumbua Mama yako, unaanza kumsumbua Mama mkwe! Unaanza kusumbua ndugu sijui hivi sijui vile!
Labda nikuambie, tabia ambazo mwanaume wako anazo sasa hivi kabla ya kukuoa ndiyo hizo hizo atakua nazo kabla ya ndoa, najua unajipa moyo lakini ndiyo ukweli, hivyo kama unamkubali mkubali na tabia zake lakini sio unaolewa uanaanza kupiga kelele kana kwamba ulikutana naye kwenye mlango wa pepo! Kama unashida sana ya ndoa olewa lakini sio unaolewa uanaanza kusumbua wamama wa watu wakati ulikua unajua! Najua unajipa moyo huyu atabadilika abadilike kwani kakuambia anashida ya kubadilika.
Sema wadada wakati mwingine mnachekesha, mtu anakunywa pombe, pombe inampa raha halafu unataka abaidilike aache pombe kisa wewe hutaki! Kwani si kuna wanaume ambao hawanywi pombe si ungewatafuta huko! Mtu ni Malaya anatoa huduma kwa marafiki zako na mabaa medi anaenjoy kabisa eti unamuambia aache kisa wewe hutaki, sasa yeye inamhusu nini kama hufurahii, au unafikiri anachepuka ili kukuridhisha wewe! Iko hivi kama huwezi kuvumilia tabia zake muache sio unaingia kwenye ndoa uananza kulalamika!
0 Maoni