DAIMA UTABAKI KUWA DHAHABU.

Kuna hali ya kukata tamaa kwa sababu ya mpuuzi mmoja tu amejaribu kuondoa thamani yako.
Haijalishi ni mpenzi,ni mke,ni mume vyovyote hata kama ni rafiki.
Tugese hapa kwenye mapenzi.
Hapa ndipo palipo na shiida,mliishi pamoja leo amekutumia haoni thamani yako tena.

THAMANI YAKO IPO KWAKO.
Haijalishi umezalishwa,haijalishi Binti umezaa ukiwa mikononi kwa wazazi,ujaolewa una mtoto/watoto,bado upo na thamani.
Naongelea in deep kwa wanawake,kwa wadada sababu ni wahanga wa kutendwa.

Tabia ya kuwasema vibaya wadada waluozalishwa kabla ya kuolewa ni upuuzi ni ushetani wa mwisho,je mimba alijidunga mwenyewe,alishukiwa na roho mtakatifu,,? ni wanaume ndio wanawabebesha mimba na kuwakimbia
Ila dada pia kua makini na mwili wako kama unaona huwezi kulea mtoto kama ukitelekezwa basi usikubali kufanya mapenzi siku za hatari
Hii pia inakufanya uonekane unajitun

Jamani mwenye mapenzi hana mbwembwe,mwenye nia na lengo na wewe wala ahangaiki ulipo au ulikotoka umepitia mangapi,wala hakupekui.
Ukiona unapekuliwa sana na mtu anaekuaminisha anakupenda,huyo muongo.





Ni muongo kwa sababu ukipenda chongo anaona kengeza,kama mkwenyezo fulani hadi raha,vinginevyo ni tamaa fulani tu akikupata ndio ''amebadilika,anitafuti tena,ana muda,yuko busy.
Yuko busy kwa sababu kuna mtu yuko busy nae.

Kuna wakati unajiuliza na watoto wangu atanitaka nani.
NO,wapo wenye watato pia wanataka kutengeneza pear,wanaweka uwiano,nina watoto wa 3 na wewe wa 3 tuwalee pamoja,maisha yanasonga.
Kuna wakati hata wazee wanaoana kwa sababu ukishakuwa binadamu umetimia,kiakili,kimwili na hisia huwezi kukwepa hisia za mapenzi,hakuna.

MWISHO.
Usijishushie thamani kwa sababu umezalishwa,uliolewa umeachwa,binti umezalishwa mwanaume kakutelekeza.
Unayo thamani,kila kitu cha wewe kuitwa mwanamke unacho,.
Mungu wa ajabu saana kama leo tungekuwa tunaachana na maungo ya miili yetu yanachakaa,au kupotea kuisha aiseeee kila mtu angomba apotee au na kupendwa tena kwishaaa.
Ila cha kufurahisha anapokuacha au mnapoachana kila mmoja anaenda na utamu wake,atakaye kuja anamkuta mpya,kwa ndani na nje kitu kipyaaaaaaa,mtu mpyaaaaaaa.

WEWE NI DHAHABU,WEWE NI WA THAMANI SANA JIDHAMINI.

Chapisha Maoni

0 Maoni