UKIMSAIDIA MWANAUME AKAFANIKIWA KULIKO WEWE NI LAZIMA AKUACHE/AKUNYANYASE KWANI HUWI TENA WA HADHI YAKE!

Image may contain: 1 person, smiling, standing


Najua hilo neno “Lazima” litawachanganya kwani kuna wakati mwingine haiwi hivyo. Lakini ukweli nikuwa mara nyingi mwanamke ukikutana na mwanaume ambaye laba hana kazi, au hana elimu, au ni mlevi ana tabia mbaya flani ambayo humfanya kudharaulika kwenye jamii, humfanya watu kumchukia na kumuona wa hadhi ya chini. Kama ukiibadilisha ile tabia, labda ukamtafutia kazi, ukamsaidia akaacha pombe, ukamfungulia biashara na kumfanya kuwa na maisha mazuri, ukamfanya kuheshimika tena.
Mwanaume kama huyu mara nyingi huja kukuacha na wanawake wenye tabia hizi za kubadilisha wanaume mara nyingi huishia kuachwa na kwenda kubadilisha wengine na wengine. Iko hivi katika mapenzi wanaume hutongoza wanawake wa hadhi zao, ni ngumu sana kwa mwanaume kumtongoza mwanamke ambaye anaona kamzidi hadhi sana kwani anajua kua atakataliwa au atamnyanyasa. Kuna wanawake wengi ambao mwanaume falani angetembea nao lakini kwakua hana pesa, hana hadhi flani hawezi kuwapata basi anaamua kutulia tu.
Kwa mfano mwanaume wa darasa la saba anatamani kuitembea na mwanamke wa chuo kikuu, anayetembea kwa mguu anatamani kutembea na binti mrembo anayeendesha Range Rover, hatembei nao kwakua hawezi kuwapata na si kwakua hataki. Sasa mwanamke kama ukijifanya mimi nampenda hivyo hivyo, ukamcuhukua mwanaume, ukaamua kumbadilishia maisha yake, ukampa thamani, akawa na pesa, akawa na hadhi basi kuna mambo mawili yatatoke. Kwanza kabisa wale wanawake waliokua wakimdharau watamuona na kumtamani.
Lakini yeye pia hadhi yake itapanda na atataka kuwapata wale wanawake ambao kwa hali yake ya zamani asingewapata. Lakini kuna jambo la tatu litatokea, ataona pia kumbe hata wewe si wa hadhi yake, aliikukubali kwakua kipindi mnaanza mawasiliano alikua na hali mbaya. Hivyo moja kwa moja ataona kuwa wewe ulikua wa kipindi kile ana shida lakini sasa anahitaji kuwa na mtu wa hadhi yake. Kwa maana hiyo dada zangu wote ambao mnawachukulia mikopo wanaume, mawasomesha, mnawatafutia kazi jueni kua mnatoa sadaka, hilo ni fungu la kumi!
Tena kama wewe ni wale akina dada ambao, wewe unafanya kakazi kako ka mshahaara mdogo tu, nataka niwataje Walimu kwa maana ndiyo wenye hii tabia ya kuchukulia wanaume mikopo. Sijui mmelogwa na nani lakini niseme tu siwezi kumaliza wiki kabla sijasikia stori ya dada Mwalimu kamchukulia mkopo mchumba wake au mume wake na katelekezwa. Sijui kwanini, lakini kusema kweli wiki haiishi kabla sijasikia Mwalimu kalizwa, labda ndiyo maana tunaambiwa tuoe mwalimu.
Naomba nirudi kwenye mada, wewe ni mfanyakazi, una mshahara wa kawaida, ukamchukulia mwanaume mkopo, ukampa akafanya biashara, akafanikiwa. Kumbuka wewe mkopo unatakwa hivyo mshahara wako kama ulikua laki nne unaweza kubaki laki mbili. Kwa maana wewe umejishusha hadhi umekua wa laki mbili, lakini yeye umempanisha hadhi umemfanya wa milioni, jua nilazima, narudia nilazima ataenda kutumia pesa zake na watu wa hadhi yake na kukaucha wewe ukipembana na hali yako.
Ndiyo ilivyo, hata kama mwanzoni alikua anakupenda, anakushirikisha katika mambo yake mnashauriana, lakini baada ya yeye kupata atawaza “Utanishauri nini wakati wewe mwenyewe maisha yako ya laki mbili!” unapompandisha mtu hadhi ambayo huna basi jua kua ataenda kuomba ushauri kwa watu ambao ni wa hadhi yake. Labda nikupe mfano mmoja, hivi kweli mtu ambaye anataka kununua gari ataenda kuomba ushauri kwa mtu mwenye gari au mwenye baiskeli?
Najua kuna ambao mtapuuza, lakini baada ya muda mtanifuata na kunilalamikia, ila kama unachukua mkopo kumpa mtu mwingine, hata kama ni mume wako, unachukua mkopo unampa ili yeye afanikiwe. Kana kwamba huo mkopo wewe ukiuchukua na kufanya biashara ndiyo itakufa. Kuna mwingine anakuambia kabisa nilichukua mkopo nikampa mume wangua kanunua gari kaandika jina lake!
Sasa ulitaka aandike jina la nani kama wewe mwenyewe hujielewi, kama wewe huwezi kuwekeza milioni kumi mpaka umpe mwanaume awekeze, huwezi kununua gari mpaka umpe mwanaume akanunue unafikiri akizipata ataacha kukusaliti. Kwanini asiende kutafuta wanawake wa hadhi yake na maisha kuendelea, sijui hata kama mmenielewa lakini ndiyo hivyo, kama una katabia haka basi jua utaishia kutelekezwa tu, huwezi kumpa mtu tiketi ya ndege wewe ukatembea kwa mguu halafu unataka msafiri pamoja.
Image may contain: 1 person, smiling, standing

Chapisha Maoni

0 Maoni