FURAHIA KUISHI PAMOJA, KULA RAHA, JILINDE KIKIPATO NA ACHA KUJIITA MKE WAKE HAJAKUOA!

Related image
Kila siku lazima nipokee simu za wanawake wawili au watatu ambao wamedhulumiwa na wachumba wao! Mwanaume amekuambia nakupenda, kakuzalisha kajitambulisha kwenu unajipeleka kwake unaanza kujiita mke! Dada yangu kwanza jua wewe si mke bali ni hawara ambaye mnaishi pamoja, huyo mtu hajaoa na inawezekana hata hana mpango wa kuoa, utajinyendekeza na hata kumlamba miguu, utajipost na kila siku kuhangaika kumnyenyekea Mama yake lakini si mume wako!
Lakini unafanya kazi, unavihela hela vyako, labda jamaa ana kiwanja chake, alinunua kabla ya kukutana na wewe au hata kanunua yuko na wewe, ameanza kujenga halafu anakuambia mchangie, au hata si yeye kakuambia, labda yeye ni falafala flani hayo mambo ya kujenga bado kabisa lakini wewe ulivyo na kiherehere ili kuonekana wife material unamshawishi mjenge, ulivyo fala zaidi, narudia fala zaidi unachukua na mkopo.
Mnatia hasira unachukua mkopo kujenga katika kiwanja cha mwanaume ambaye hata kukuoa hataki, unamfumania kila siku una kazi ya kuwa customer care kila siku kuwapigia wanawake zake kuwaambia chana na mume wangu! Mume kakuoa! Mtu kakufanya mdada wakazi ambaye anakutumia kingono tu, hakujali, anachepuka tena waziwazi eti kwavile unamfulia na kumpikia unajiita mke na kujenga unamjengea! Naomba niwaulize hivi nani aliwadanganya kua mkijenga nyumba zentu wenyewe zitageuka mawe?
Niujinga! Niujunga! Niujunga! Kama mtu hamjafunga ndoa, hamtamuliki kisheria kujenga, kununua gari, kufanya chochote ambacho hakika jina lako ni ujinga! Hata kama mmeishi pamoja miaka 100 bado ni ujinga! Kama angekua anakupenda, anakuamini basi angekuoa, kwani ndoa ya skierikalini bei gani? Si Shilingi elfu hamsini tu! Narudia huyo mtu si mume wako hatata kama amekutambulisha mpaka kwenye makaburi ya Babu zake! Nakereka sana binti umetafuta pesa kwa shida halafu unakuja kudhulumiwa kindezi ndezi wakati unasoma post zangu jifunze!
NB; Nataka mkasirike muache huu ujinga maana mnatia huruma mnavyojiozesha wakati mwenyewe bado anatafuta mchumba! Kama unaishi naye ishi naye furahia tendo la ndoa, furahia kutokua mpweke lakini kamwe usijidanganye kuwa ni mume wako eti chake chenu, hapana si mume wakoa anaweza kukuacha dakika yoyote na kuoa mwingine. Jilinde kikipato!

Chapisha Maoni

0 Maoni