KUA MAKINI SANA HUYU SI MAMA MKWE NI MJASIRIA MALI!

Related image

Kama una mchumba wako, alishakutambulisha kwao na ndugu zake wanakujua, wanajifanya kukupenda, umefika kwa Mama mkwe siku moja tu na kumpa namba yako ya simu lakini anakupigia simu na kukujali mpaka unaanza kuwa na wasiwasi kama Mama yako mzazi ni Mama yako kweli au alikua ni Mama wakambo, maana anajali mpaka basi, anapiga simu na kukuhakikishia kua wewe ndiyo mkwe wetu sijui nini na nini?
Lakini haishii hapo utasikia Mama na mimi nilikua naumwa hela ya dawa sina, sijui mwanangu hivi na vile, mwanangu kimependa kimeshuka, kumeinama kimebiduka, yaani umetambulishwa tu lakini Mama mkwe anaanza kukuomba pesa, tena wengine si Mama tu na ndugu wengine yaani wanakuona kama vile ushaolewa na wako huru kabisa kuomba pesa. Ndugu yangu huyo si Mama mkwe ni mjasiriamali, narudia hapo hakuna upendo bali ni huduma kwa wateja.
Ushawahi kuwapigia wale wa dada wa Tigo, au Voda, wanavyokuongelesha vizuri wanakusalimia na kukujali, unadhani hata wanakupenda hapana ni kwakua umteja na unanunua vocha wanapata mishahara! Basi huyo ndiyo huyo Mama mkwe wako. Lakini haishii hapo labda mwanaume wako ni kichomi, anachepuka na ana wanawake wengi, tena mwingine hata akishakuambia hatakuoa amemtambulisha na huyo mwanamke mwingine.
Lakini Mama mkwe anakuambia “Sisi tunakutambua wewe hao wengine anawachezea tu!” Hahhahahahha! Unajua naandika huku nacheka mpaka najiona chizi... Dada yangu hiyo familia ya wasanii unaibiwa! Narudia unaibiwa, siku ukiacha kutoa pesa basi jua familia nzima inakununia! Lakini siku huyo kijana wao akipata mwanamke mwenye pesa zaidi yako utatelekezwa kana vile umebeba furushi la Mavi. Hivyo kuwa makini na wakwe kama hawa, acha! Acha! Acha! Acha kabisa kutoa pesa, kwanini ununue ndoa.
Familia inayojielewa wanamuomba pesa mtoto wao si mkwe! Narudia kama Mama mkwe wako, wifi zako, shemeji zako wanakuomba pesa kila siku na wengine usipo wapa wananuna dada yangu hata ukiolewa jua hakuna ndoa hapo, nilazima ujifunze kusema hapana, wanune na kununa lakini si jukumu lako kununua ndoa! Najua unatamani sana kuolewa na utaendelea kutoa pesa hutaniamini. Ila kama ninavyosema wewe katoe pesa wasomeshe mpaka na wajukuu zake akikuacha njoo hapa tuweke kisa chako uwe ‘Shamba Darasa kwa wengine!”

Chapisha Maoni

0 Maoni