KAMA UNAUMIZWA NA MANENO YA MWANAUME WAKO HEMBU SOMA HAPA KIDOGO!

Related image
MTEJA; Hivi Kaka Iddi kwanini unazungumzia sana kuhusu wanawake kujipa fuaraha wenyewe na si wanaume kubadilika?
IDDI MAKENGO; Nina sababu mbili, sababu ya kwanza nikwakua mwanaume kubadilika ni maamuzi yake na yeye tayari ana furaha yake kutokana na tabia yake, kwa mfano kama anachepuka inamaana anafurahia kuchepuka kwake, kama anakunywa pombe anafurahia pombe yake na kama anampiga mke anafurahia kumpiga.
Kwa maana kuwa yeye tayari kashaamua aina ya maisha anayotaka hivyo huwezi kumbadilisha kwa vilio. Sababu ya pili nikuwa kinachowaumiza wanawake si mapendo ya wanaume bali ni namna wanavyoyachukulia matendo ya wanaume, ule upweke na ile hali ya kushindwa kujipa furaha zao wenyewe ndiyo zinawaumiza.
MTEJA; Sijakuelewa, inamaana unataka mwanaume akichepuka na mwanamke naye achepuke?
IDDI MAKENGO; Hapana simaanishi hivyo, wanawake siku hizi wanachepuka tena pengine kuliko wanaume, lakini kuchepuka kwa kulipa kisasi hakumpi mwanamke furaha hata siku moja. Ninachomaanisha ni hivi, tuchukulie mfano, mwanamke mume wake anachelewa kurudi nyumbani, maumivu ya mwanamke hayatokani na kuchelewa bali hutokana na kusubiri.
Ule muda ambao mwanamke anakaa tangu watoto wanalala mpaka mwanaume anarudi, zile simu ambazo anapiga kuulizia umefika wapi anasikia makelele ya walevi ndiyo wakati ambao wanawake huchanganyikiwa. Sasa mwanamke wa namna hii kwanini asijifunze kulala. Mfano mwingine, mwanaume anaweza kuchepuka mara 100 lakini kinachoumiza si mwanaume kuchepuka bali ni mwanamke kujua.
Sasa kuna wale wanaume wanafanya makusudi ili wajulikane, lakini hembu fikiria, mwanamke anahangaika kutafuta password ya mwanaume, anaiona anaona picha za uchi, anauliza anapogwa kwa kugusa simu na kesho yake mwanaume ananuna siku mbili mwanamke anaumia tena analazimika kumuomba mwanaume msamaha ili tu asinune. Baada ya wiki anafumania tena, anapigwa, mwanaume ananuna tena mwanamke anaomba msamaha.
Sasa swali la kujiuliza hapa ni hivi? Kwanini huyu mwanamke anahangaika na simu ya mumewe wakati anajua anachepuka na atakuta meseji za wanawake wengine? Lakinia najua kabisa, atakuta na atapigwa kwa kukuta ila bado anatafuta! Hiki kinachomsukuma kuchokonoa ndiyo ambacho mimi na dili nacho. Lakini kingine kwanini mwanamke kafumania, kapigwa, mwanaume kanuna huyu huyu mwanamke anaomba msamaha?
Huyu mwanamke unajua anaumizwa mara mbili, kwanza na kuchepuka lakini pili na mnuno! Siwezi kumzuia mume wake asichepuke, hiyo dawa sina, ila naweza kumsaidia asiumizwa na mnuno wa huyo mwanaume na kikubwa asihangaike na simu ya mwanaume. Labda nikupe mfano mwingine, mwanamke anatukanwa, anaambiwa ananuka, anasura mbaya, hana matako na kila kitu!
Lakini ukiangalia wala hanuki, hata kama hana wowowo lakini hata kabla anatongozwa hakua nalo sio kwamba limeyeyuka, sasa kwanini uumizwe na maneno kuwa huna wowowo wakati unajua kabisa halipo? Kwanini uumizwe na maneno kuwa unanuka wakati unajua hunuki unanukia kama umemeza Deodorant! Lakini wanawake wanaumizwa, sasa katika kitabu changu kujipa fuiraha ni pamoja na kutokuumizwa na kutoumiwa na matendo ya mwanaume bila kujali ukubwa wake.
Hiii ndiyo maana nasisitiza furaha yako mwenyewe kwamba matendo ya mtu hayakuumizi kwakua wewe mwenyewe unajitambua. Mfano mimi leo nikapita mtiu akaniambia fala wala sitaumia kwakua najua mimi si fala, akiniambia nanuka sanasana nitamuambia ziba pua hata kuoga sitaoga kwakua najitambua na maneno ya mtu wala matendo yake ni yake hayanites

Chapisha Maoni

0 Maoni