
Unajisikiaje yule umpendae anakufanyia jambo ukulitegemea kufanyiwa.
Hakuwa na kawaida hiyo ni kama mshtuko kwako,yaani mpaka kichwa kinaweweseka,kinasisimka kwa furaha na bashasha,hiyo ndio nguvu ya SPRAIZ.
Inarudisha hisia zilizoanza kupotea.
Hisia ndio kiini cha Mapenzi,bila hisia hakuna Mapenzi,unajipunja,unajipotezea Muda.
Inachekesha sana,kuna watu wanaingia kwenye mahusiano hawana hisia kwa mtu anayekwenda kuwa Mume kuwa mke,Mbaya sana.
Ulikuwa mtu wa kupotezea vitu vidogo vidogo,vidogo ndiyo vinaua hisia na ndiyo vinalinda na kuamsha hisia,usipuuze wala kuvichukulia poa.
Unaishi na Mume na Mke unachukulia poa mwenzio akikuambia amekumiss,kaneno kadogo sana ila ndio uhalisia na kiini cha upendo.
Akisema nimekumis kuna kitu kimemgusa ndani ya moyo wake na furaha yake asikie kutoka kwako unajibu nini baada ya kukutamkia "NIMEKUMIS MKE/MUME.
Ukichukulia poa,unakwenda kuondoa taratibu hisia zake kwako,lina thamani usilipuuze.
Utaongeza chachu kwa kulichukulia kwa uzito wake na utashangaa hisia zikiwa zinaboreka.
SPRAIZ kwa zawadi,kwa out,kwa faragha.
Kuna watu leo Mwaka unaelekea ukingoni,Tukijaaliwa uzima,hata siku moja ajawahi Kumspraiz mke wake,mume wake hata upande wa Kanga,Hata Sidiria,Hata Under ware kwa mkewe.
Hata wa mama Mwaka unakatika awajawahi kuwaspraiz waume zao hata kwa T-shat,Boxer,Saa,soksi,Jamani hata za bei poa na uzuri wa zawadi haijalishi ya Ghali hata ya Chee poa tu.
OUT,kutoana out kwa wawili kwa familiy,haijalishi kipato kikubwa au kidogo.
Unaamua tu mwisho wa mwezi mmoja unatenga kiasi kidogo,mshtukize mama au kwa Family kutoka out week end moja au hata siku za kawaida jioni Dinner inaliwa nje ya nyumbani,iwe Mgahawani,Bar au Hotelini,ni wewe na uwezo wa kipato chako.
Spraiz ya Faragha,,Mmmmmmh,! kama mnapakodolea saaana.
Kwa sababu ndipo patamu,ndipo makao makuu ya Ndoa,hakuna ubishi bila sex hakuna ndoa na kama itakuwepo ya bora tuishi kulea watoto.
Tunaishi kwa kuzoeana kwenye tendo hakuna ubunifu,Toka mwanzo wa ndoa mambo ni yale yale.
Embu mshtukize urudishe hisia zake,hisia zinarudi haraka kwa kuacha mazoea.
Msiseme sijasema
0 Maoni