Stori za kuishi na Mume/Mke kwenye mahusiano na hana msaada kwako,ni Hadithi binafsi kwangu nimezizoea saana.
Oooh Mume wangu msumbufu,ananitesa,michepuko mpaka ndani,toka tumenza kuishi ni kunuliza tu,sijawahi kuifurahia ndoa yangu.
Kadhalika hata wanaume wanakuja kulalamika wanasumbuliwa na wake zao,wasumbufu,hawana mapenzi,ni wababe,wanapunjwa na haki ya Ndoa n.k.
Ukija kuuliza wana miaka 10 na zaidi kwenye ndoa kwenye mahusiano.
NI BORA KUAMUA KUISHI PEKE YAKO KWA AMANI.
Ni bora mpweke peke yako kuliko kuwa mpweke na mtu,mtu ambaye unamtegemea kukufariji laki anakulaza na hasira kila mara,ana kutoa machozi na huna wa kukufuta.
Wakati mwingine akili inachoka kwa sonona za mara kwa mara,kuanzia asubuhi,mchana mpaka jua linatua huna amani,ikitokea kulejea nyumbani unawaza nini kitazaliwa.
Mmeyapeleka kwa wazazi,kwa ndugu kusuluhisha mpaka wanachoka.
kwa wazee wa mabaraza,Bakwata nako hakuna suluhu.
Unachelewa kuamua basi,unawaza watoto,unawaza unaishije,unawaza watanicheka.
Sasa unakubali moto ukuunguze sababu watoto,na wakati mwingine watoto wanakutaka muondoke,watoto wanaumia hali mnayoishi.
Unaishi kwa maamuzi kisa ndugu,majirani wataema nini,,hapana tengeneza kesho yenye amani na furaha.
Juzi kuna rafiki yangu tumejuana kitambo sana,kujuana katika mazingira ya kushauriana.
Ndoa yake haikuwa yenye amani kiukweli,ni vurugu mwanzo mwisho.
Huku na kule hakuna amani,alijifunga moyo mkanda akaamua iwe basi,iwe imetosha.
Kilichopo sasa anaenjoy life kwenye mahusiano,amempata mtu mpaka anashangaa kwa nini alipoteza muda kwa mtu msumbufu.
Hajawahi kupendwa namna hiyo,kumbe wapo watu wanajali wanathamini,wana utu wacha Mungu.
USIOGOPE KUFANYA MAAMUZI,ILI KESHO YAKO IWE YA FURAHA NA AMANI.
0 Maoni