JE, MWANAUME ANAWEZA KUNIAMBIA TUZAE NAYE AKIWA HANA MPANGO WA KUNIOA?

Related image

Najua akina dada mnajiuliza hili swali, upo kwenye mahusiaho Bambam, mnapendana paka basi. Mwanaume anakuja mpaka kwenu kujitambulisha au wakati mwingihe haji kujitambulisha rasmi lakini mnamahusiano mazuri, simu yake unashika kama yako, haina Password na kila kitu ni kizuri. Anakuambia kuwa nataka kuzaa na wewe, unamuambia aje kwenu kwanza kujitambulisha akuoe. Anakupa majibu ya namna hii ambayo wewe unayaona matamu. (1) Umri unaenda, sasa hivi najipanga mpaka mwezi wa sita nataka nikija kwenu nishamalizia nyumba na tuna mtoto tayari, nataka kuzaa kwanza halafu nitakuja. (2) Nataka ubebe mimba ili iwe rahisi mimi kuja kwenu kujitambulisha wasije kunikataa. Pengine anatoa mfano si unajua kwenu kabila flani wanaweza kataa, au dini flani wanaweza kukataa. (3) Siwezi kuoa mwanamke ambaye sijajua kama anaweza kuzaa au bado (hili ni jibu la kishenzi) nataka ubebe mimba kwanza ndiyo nije kwenu. (4) Mama yangu ana hamu ya mjukuu, na mimi pia nina haraka naye, nataka ubebe mimba kwanza. (5) Kwetu wamekukataa kwasbaabu ya dini/kabila ila ukibeba mimba nina uhakika watakubali.

Dada anakupa majibu mazuri mpaka unatamani uwape wanafunzi wa kidato cha nne wayatumie labda wangepata ONE, kwa taarifa yako asilimia 60 ya single mother walikua kama wewe. Walikua hawajui kama wanaweza kuachwa, yaani walikua wanapendwa mpaka Njiwa wanaona wivu. Lakini ukweli mwingine nikuambie, sasa ukubali usikubali!

Asilimia kubwa ya wanaiume wanaotaka uzae wanakua natumia hiyo kauli kama kauli ya kukufanya wewe ukate tamaa kua naye ila nyie wadada mnaitafasiri kinyume anakuambia hivyo ili kama unaakili useme siwezi ukisema huwezi ili achukue kama sababu ya kuachana kwamba mlishindwana ili umwache na pia wanakuaga wanawake zaidi ya mmoja, yaani wakati anakuambia zaa kuna mwingine nayeye anaambiwa zaa. Na nikuambie, huwezi kumjua mpaka una mimba, yaani sijui ni shetani anawasidia kuficha lakini ukiongea na single mother wengi walijua jamaa zao wanachepuka baada ya kubeba mimba. Sasa kama una akili basi jibu unalo.👌👌ILA MABAHARIA SAMAHANINI SANA KWA HAPO KAMA NITAKUWA NIMEWAUDHI👏

Chapisha Maoni

0 Maoni