Umuhimu wa uzuri wa nje wa mwanamke hauwezi kuwa sawa na uzuri wake wa ndani. Uzuri wa nje sio msingi wa kuyang’arisha maisha ya ndoa, kwa sababu uzuri huondoka baada ya umri kusonga, na kinachobaki ni muamala mzuri. Mwanamke hana budi kuwa na usafi wa moyo katika kushirikiana na mumewe kwa sababu watakutana na matamu na machungu ambayo wanatakiwa kukabiliana nayo kwa kuridhiana na kuridhika pia. Wanatakiwa kuzikabili changamoto na kushirikiana vipindi vya huzuni bila kulaumiana wala kukata tamaa, hapo yatapatikana maelewano kati yao.

0 Maoni