Mtu wa kwanza kabisa anayetakiwa kuchukua hatua

“Mtu wa kwanza kabisa anayetakiwa kuchukua hatua maridhawa za kuepusha mgongano kati ya mke na mama mkwe ni mume mwenyewe. Mume anatakiwa kutengeneza mapenzi mazuri kati ya mkewe na mama mkwe na kuwafanya wapendane. Iwapo hatochukua hatua hiyo, akapendelea kuegemea upande wa wazazi wake wenye msimamo hasi dhidi ya mkewe, hapo mke atagundua haraka sana na kuchukua hatua za kujihami, jambo ambalo litamfanya awe na chuki dhidi ya wakwe zake, hali ambayo itaibua mgogoro na ugomvi. Hali itakuwa mbaya zaidi iwapo mume hatokuwa makini akaenda kuwaambia ndugu zake kila linalotokea kati yake na mkewe, jambo litakalofanya familia za pande mbili kuibuka na kila moja kuuhami upande wa mtoto wao.”

Chapisha Maoni

0 Maoni