ishukuru sana familia yake, iheshimu familia yake na epuka maneno ya shombo kwa familia yake

ishukuru sana familia yake, iheshimu familia yake na epuka maneno ya shombo kwa familia yake. Hata kama yeye mwenyewe hapatani nayo lakini bado kumbuka kuwa ni familia yake.
Mara nyingi wanaume tunataka kuwa wake zetu kupatana na ndugu zetu, wake zetu kuwaheshimu mama zetu na wake zetu kuziheshimu familia zetu lakini hatuoni umuhimu wa familia za wake zetu.
Mwanamke akionekana kujali hata kidogo tu familia yake anaonekana kama anafanya kosa, kama anataka kukutawala na kama anataka kuhamishia mali zote kwao, tunaona kama familia zetu zinahaki zaidi kwetu kuliko familia zao.
Kumbuka tu kama unavyoipenda familia yako, unavyoijali na unavyoitegemea ndivyo nayeye anavyohisi kwa familia yake. Usimtengenezee mazingira magumu ya kumfanya kushindwa kupatana na familia yake.
Mwanaume hana haja ya kumshusha mwanamke, hana haja ya kumuonea wivu mkewe, hana haja ya kumdhalilisha mkewe mbele zawatu, hana haja ya kumnyanyasa na kumfanya ajisikie vibaya.
Mwanaume anajua kuwa yeye ni kiongozi na anajua kua anategemewa, anajiamini vyakutosha na hahitaji kumshalilisha na kujaribu kumshusha mwanamke ili yeye kujiona yuko juu.

Chapisha Maoni

0 Maoni