
Bibi wa miaka 80 alikuamekaa chumbani kwake akilia, ni wiki moja baada ya kumzika mumewe wa miaka 85 ambaye walidumu naye kwenye ndoa kwa miaka 63. Wajukuu zake waliingia na kumbembeleza wakimuambia asihuzunike kwani Babu yupo sehemu salama na wao watamtunza. Huku akifuta machozi Bibi alisema “Matiti Yangu Wajukuu Zangu”
Wajukuu walistuka kwani hawakua wakijua anamaanisha nini. Bibi aliwaambia Babu yenu alikua ananipenda sana lakini alikua anapenda zaidi matiti yangu. Katika miaka yetu yote ya ndoa aliyaangalia Matiti yangu kama siku ya kwanza aliyoyaona, pamoja na kumzalia na kunyonyesha watoto kumi lakini kwake matiti yangu yalikua ni kama yale ya binti wa miaka kumi na saba tulipoana.
Siku zote sikujihisi nimezeeka kwani macho yake kifuani kwangu yalinikumbusha ujana wangu. Sasa nalia sio kwasababu Babu yenu amekufa hapana. Najua yuko sehemu nzuri lakini nani atayaangalia tena matiti yangu kwa kama yeye alivyokua anayaangalia, wiki moja tu babu yenu kafariki najiona nimeshazeeka tayari. Wajukuu walibaki kimya hawana chakujibu. Je wewe bado unamuangalia mkeo kama ulivyomuangalia siku mliyokutana? #SHARE
0 Maoni