Kwa Mwanamke Upendo Nilazima Uonyeshwe, Acha Kumkataa Mbele Za Watu!

Image result for african beautiful

Kama wewe ni wake atataka kuonekana mbele za watu kuwa kweli ni wake na raha ya mapenzi sio nyinyi kupendana tu bali na watu pia kuona kua mnapendana. Kwa mwanamke hili ni la muhimu ziadi kuliko kwa mwanaume. Kwa maana hiyo basi inauma sana kwa mwanamke anapokua na mpenzi wake mbele za watu akataka kumshika mkono na kufanya kitu chochote cha kuonyesha kuwa yeye ndiyo mmiliki wa yule mwanaume na mwanaume akakataa.
Kuna wanaume utawasikia wakisema cha amambo yako, sipendi ujinga huo. Mambo gani hayo ya kushikana shikana, si utangulie kwani ni lazima tuongozane na maneno mengine kama hayo ili tu kumfanya mwanamke kutokuonyesha kua wako pamoja. Kama mwanaume unatakiwa ujue kuwa hilo linauma sana na linakera, kwanza unampa ujumbe kua humpendi vyakutosha kiasi cha kuonyesha mbele za watu kua mnapenda na na pili unaonyesha kuwa inawezekana kuna mtu mwingine anakumiliki ndiyo maana hutaki muonekane pamoja.
Wewe unaweza kuona kama kitu cha kawaida, ukachukulia poa lakini kwake ni kuonyesha utawala, kutangaza kuwa yeye ndiyo mmiliko hivyo wengine wakae pembeni. Kitendo chako cha kukataa kuonyesha mapenzi yako mbele za watu kwake ni ishara kuwa kuna kitu unaogopa, labda unamsaliti au kuna mwingine hivyo hutaki ajulikane.
Maumivu yake ni zaidi ya usaliti wenyewe kwani mbali na kuhisi unamsaliti lakini pia atahisi hujisikii vizuri kuonekana kama wapenzi mbele za watu. Ataanzakujiangalia kama vile ana kasoro, kama vile ni mbaya ndiyo maana hutaki kumuonyesha kwa watu. Hivyo kuwa makini, hata kama ni vitu ambavyo hupendi nibora kumuambia mapema kuliko kumkataa mbele za watu, lakini pia hata kama ulishawahi kumuambia kuwa hupendi tabia hizo akikuonyesha huna haki ya kumkatalia mbele za watu.
Kwanini uruhusu vitu vidogo kama kushikana mikono, kuitwa Baby, kusifiwa mbele za watu, kushikwa bega, kutengenezwa shati na vitu vingijne vya kimahaba kama hivyo viharibu ndoa yako, vimfanye mkeo ajisikia vibaya kama vile hana thamani. Aone kama unamkataa mbele za watu kwakua labda una mtu mwingine unampenda na hutaki aone au kwakua unaona kua hana thamani ya kuwa mtu wako hivyo unakwepa kuonyesha unampenda mbele za watu?
#BADILIKA

Chapisha Maoni

0 Maoni