KISA CHA RAFIKI YANGU; Msaidie Mume Wako Kuwahi Kurejea Nyumbani!

Image result for african beautiful


Miaka miwili iliyopita rafiki yangu mmoja alinifuata kuniomba ushauri au niseme kunilalamikia. Ni katika kipindi ambcho nilishamaliza kuandika kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu”. Kikiwa na mambo mengi niliyokuwa nimeandika nilitamani kumsaidia kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni rafiki yangu hivyo niliona kama wajibu wangu kufanya hivyo na pili ni kwaajili ya kitabu changu.
Kwa kawaida huwa napenda kuandika, hivyo naandika mambo mengi lakini naamini Ili mambo ninayoandika yawe Na maana nilazima niyaweke kwenye maisha ya uhalisia, kwamaana kwamba kila nadharia niliyoiandika basi iwe kwa vvitendo. Tatizo lile la rafiki yangu nilishalindika katika kitabu changu hivyo lilihitaji kufanyiwa kazi. Rafiki yangu yule wa kike ndiyo kwanza alikua na miezi mitano katika ndoa yake lakini tayari ilishaanza migogoro.
Mume alishaanza kuchelewa kurejea nyumbani, walishaanza kugombana kwa sbabau hiyo, mume alishaanza kumdharau na baada ya kuongea na wazazi wake walimuambia vumilia tu ndiyo ndoa zilivyo. Kwanza baadhi ya ndugu walimshangaa kulalamikia kitu kama kile, kwamba kwao mwanaume kurejea saa nne usiku bila sababu yoyote ya msingi lilikua ni jambo la kawaida ambalo mwanamke alipaswa kuvumilia.
Walimnanga kwa kumuona kama si mvumilivu na kuona kwamba kama ataendelea hivyo basi ndoa itamshinda. Kama rafiki yake alikuja kwangu kuomba ushauri akiuliza kama alichofanya ni kitu kibaya kuwaambia ndugu. Sikumjibu swali lake kama alichofanya ni kibaya au la lakini niliamua kutumia kitabu changu kumsaidia. Kwamba sikutaka mambo ya kuvumilia bali nilitaka ambadilishe mumewe ili wote wawe na furaha.
Sasa najua kuna wanawake wengi ambao hili ni tatizo na kusema ukweli katika ndoa nyingi hiki ndiyo huwa chanzo cha migogoro mingi. Mwanaume huanza kuchelewa, mke huwa mkali na hatimaye hugombana mazima. Kwanini Wanaume Huchelewa Kurejea Nyumbani?; kama unataka kuiabdilisha hii hali ni lazima wkanz aujue kwanini wanaume wengi huchelewa kurejea nyumbani, ukiacha sababu za kikazi kwamba yuko bize kweli kuna sababu nyingine moja tu ya mwanaume kuchelewa kurejea nyumbani.
Sababu hii nikuwa huko aliko anafanya kitu kingine cha kumpa furaha au anakua na angalau kafuraha kuliko akiwa nyumbani. Hapa kuna mawili, kwanza inawezekana huko aliko anafanya mambo ya kumpa furaha. Labda anachepuka Na anfurahia, anakunywa Na marafiki, anangalia mpira Na michezo mbalimbali, lkaini jambo la pili nikwamba anakwepa huzuni za nyumbani, kwamba hataki kurejea tu nyumbani kwakua hakuna amani.
Hii ikimaanisha kuwa kama nyumbani hakuna amani inamaanisha kua huko aliko hata kama hafanyi chochote lakini angalau anafuraha kuliko kubaki na kelele za nyumbani. Kwa maana hiyo basi nilimuambia rafiki yangu yule bila kujali sababu badala ya yeye kuvumilia kwamba mume labda ipo siku atabadilika anaweza kumbadilisha kwa kumtafutia mume kitu cha kufanya nyumbani ambacho kitampa furaha zaidi.

(1) Tengeneza Amani Ndani Ya Nyumba;

Hiki ndiyo kitu cha kwanza ambacho nilimuambia akifanye, kwamba kwa sasa kuna migogoro, hivyo mume akirudi wanakua wamenuniana. Hali hii haiwezi kuabdilisha chochote hata mkipelekwa kwa viongozi wa dini achilia mbali ndugu. Labda nikuambie kitu kuhusu wanaume, wao hawapendi maneno maneno hata kama ndiyo wameyasababisha wao.
Kwamba wanataka mambo yaishe tu harakaharaka, hivyo kama hayaishi njia rahisi ni kukwepa tatizo badala ya kulisuluhisha. Sasa nilazima kuwe na mmoja wa kujishusha na kama mwanamke unaipenda ndoa yako jishushe. Acha kulalamika tena anapochelewa, ongeanaye vizuri, mpokee na jifanye kama hakuna hilichotokea. Najua utajiuliza kwanini asifanye yeye mwanaume?
Hawezi kufanya ndiyo maana anakwepa kuwahi kwakua hataki maneno na wewe. Nilazima kuwe na mtu mmoja wa kupigania ndoa na huyo mwanzoni ndiyo anapaswa kufanya kila kitu. Niliongea naye na kumuelewesha akakubali kua atakua halalamiki tena kuhusu kuchelewa kwake hata akirudi asubuhi. Hii inasiadia kuleta amani kitu ambacho wanaume wengi wanakitaka ndani ya nyumba, kiasili wanaume wanashindwa kuvumilia mtu akilalamika sana, humfanya mwanaume kujihisi mkatili kama anamuonea mtu.

(2) Mpe Majukumu;

Mtengenezee mume wako kitu cha kufanya anaporudi nyumbani, kwamba asirudi na kukaa tu akaboreka, wakati mwingine mwanaume huona kuliko kurudi nyumbani kugombania rimoti na watoto bora abaki mtanai na marafiki. Hembu fikiria anarudi nyumbani saaa kumi Na moja, anakaa mpaka saa tatu bila kuwa Na kitu cha kufanya akisubiri chakula, lazima ataboreka. Kuna mambo mengio ya kufanya ndani ya nyumba mabayo unaweza kumtumia mumeo kuyafanya.
Kuna kazi nyingi ndogo ndogo ambazo mwanaume anaweza kusaidia kufanya, kusogeza meza, kusogeza ndoo za maji, kuingiza vitu ndani, kutengeneza taa, jiko na vitu kama hivyo. Zinaweza zisiwe kazi za kila siku lakini angalau awe anasaidia. Kama mna watoto basi ndiyo raha zaidi, awasaidie homework, kusaidia kuwabeba na vitu kam ahivyo. Muhimu ni asikae tu, ajione kama anatumika anapokua nyumbani. Isiwe kila siku lakini angalau atumike. Kwamba unapomuambia awe anawahi ajue anawhai kufanya nini na si kuwahi kuangalia TV au kujifungia chumbani. Awe na wajibu falani ambao unamlazimisha kuwahi.

Chapisha Maoni

0 Maoni