
WAKATI WA DHIKI NI KIPIMO HALISI CHA MAPENZI YA KWELI
Upendo wa dhati hujidhihirisha pale inapotokea mkeo/mmeo/mchumba au mpenz wako kabadilika ghafla kutokana na mazingira yaliyomsibu kisha ukaamua kwa moyo wote kumvumilia kumfariji kumuombea na kumtia moyo katika kipindi hicho kigumu, hakika atajivunia kuwa na wewe, hata kama anayoyapitia ni mazito atayaona mepesi atasonga mbele kwa matumaini na nguvu mpya, hayo ndio MAPENZI MUBASHARA.
Ila itapotokea mpenz wako yupo kipindi kigumu alafu wewe unaishia kumlaumu tu na kumhoji mbona kabadilika n.k hakika utamvunja moyo na kumkatisha tamaa hata kama mapito yake ni mepesi aone mazito maana faraja yake alitarajia toka kwako wewe maana ndio kipenzi cha moyo wake, akiamini wakati wa dhiki na faraja pembeni yake utakua wewe kumfuta machozi kumfariji na kumtia moyo.
Wahenga husema RAFIKI WA KWELI HUJIDHIHIRISHA WAKATI WA DHIKI, upendo wa dhati ni kama kiapo baina ya wawili walioamua kuishi kama ndugu tena mwili mmoja ndio maana katika zoezi la kufunga ndoa huwa mume na mke lazima wakiri na kuapa kuwa WATAPENDANA NA KUVUMILIANA WAKATI WOTE KWENYE RAHA NA DHIKI.
Ni jambo la kusikitisha sana pale inapotokea unamdharau mwenzi wako kisa kafilisika, kafukuzwa kazi, katumbuliwa vyeti feki, kaugua ugonjwa usiotibika n. k hakika inauma sana maana kitendo hicho ni USALITI MKUBWA na dhuluma dhidi ya uaminifu aliokua ameweka juu yako akijua kuwa wewe ni wake wa shida na raha kumbe wewe ni wa raha tu mda wa shida huna mpango nae.
Waswahili husema, "Filisika tujue tabia ya mkeo" wakimaanisha siku zote mke chuma ulete aliekupendea pesa na mafanikio yako siku ukidumbukia katika matatizo na majanga lazima akugeuke na kukukimbia au kukusaliti kabisa hapo ndipo utakapojua ulifikiri waishi na kondoo kumbe chui mkali.
Usia wangu kwako unaesoma ujumbe huu,
Kabla hujamhukumu na kumchukia mtu mliyependana kwa mda kisa anaonekana AMEBADILIKA, ni vema ukatafakari mazingira na kipindi anachopitia sasa hivi na mlivokua awali, kama havifanani basi HAJABADILIKA, daima mtu wakati wa dhiki hawi sawa na alivyokua ule wakati wa furaha.
Kabla hujamhukumu na kumchukia mtu mliyependana kwa mda kisa anaonekana AMEBADILIKA, ni vema ukatafakari mazingira na kipindi anachopitia sasa hivi na mlivokua awali, kama havifanani basi HAJABADILIKA, daima mtu wakati wa dhiki hawi sawa na alivyokua ule wakati wa furaha.
Kama umenielewa SHARE post hii na marafiki
0 Maoni