Kiapo Wakati Wa Ndoa



KIAPO

Unavosema kwa kinywa chako 'Ndio nakubali' unamaanisha kwamba; sasa hivi nimekua mtu mzima, matured enough, nimejizatiti kuwa na mpenzi mmoja tu ambae ndio huyu.

Inamaanisha kwamba, sitatizama au kufuatilia mtu mwingine pembeni hata kama ni mzuri, ana pesa, handsome au ana mvuto kiasi gani.

Ina maana kwamba, Nampenda Mungu, napenda na ninamheshimu mpenzi wangu na nina mtunuku uvumilivu katika kila aina ya jambo ambalo lina uwezekano wa kutodumu nalo, iwe pesa, afya ama uzuri. Hii ndio maana ya kiapo.

Basi Nawatakia kila kheri wote walioaga ukapela leo hii kwa kufunga Ndoa, nawatakia baraka na kheri walioko kwenye Ndoa hivi sasa, Mungu awape moyo wa uvumilivu ulioshiba upendo.

Na sisi ambao bado, Mwenyezi Mungu akatuongoze vema katika kipindi kigumu kabisa cha kutambua ni nani haswa mtu sahihi, na ni nani ni mwivi au jipu ili litumbuliwe mapema!

Kwanini tusisithibitishe sala hii kwa kusema AMEN!

Chapisha Maoni

0 Maoni