Tabia Ya Kuchagua Wapenzi



Wakati tukiwa marafiki wa kawaida bado hatujaanza mahusiano na kuingia katika Ndoa, mke wangu Rachel aliniambia anapenda sana wanaume ambao ni wembamba halafu warefu.

Mimi nilimueleza kwamba ninapenda wanawake ambao wamenizidi umri kidogo na ni wafupi.

Hakuna hata mmoja wetu mwenye sifa tulizozitaja, mimi ni mfupi, na mke wangu nimemzidi miaka miwili, ila tukajikuta tukipendana na kuamua kufunga ndoa takatifu.

Tunaishi kwa furaha mwaka wa tano huu tukiwa na watoto wawili. Point yangu ni kwamba muda mwingine 'type yako' ndio sababu upo single au unaumizwa na mapenz mara kwa mara.

Stop being too selective na kuweka vigezo vingi kama fomu ya mikopo ya benki inayokaribia kufirisika. Vigezo vikubwa ni Ucha Mungu, Bidii, juhudi, hekima na maarifa. Anayemcha Mungu, siku zote hufahamu nini maana ya upendo, na hutambua kwamba Usaliti ni dhambi mbaya.

Amezungumza vyema?

Chapisha Maoni

0 Maoni