USIUMIE KAMA HAKUPENDI

Related image

Usiumie kama hakupendi.ngoja niweke hili jambo vizuri kidogo.yaani ni bora uone kabisa huyo umpendae hakupendi kuliko ajifanye anakupenda kumbe hakupendi.maumivu yake ni makali huwezi amini.

Kuna watu wakiachwa huwa sijui kwanini wanalia?naelewa ni maumivu lakini ngoja nikuambie kitu.kabla hujaachwa kuna vitu fulani au viashiria kuwa umeanzwa kuchokwa.sikiliza ukiona mtu kaaanza kukuchoka anza kujitoa mapema kabla hajakuambia.iko hivi ukiona mawingu unajua kabisa kuna mvua.

Usitake mpaka mtu akuambie hakutaki.jiachie.siku hizi hauambiwi umechokwa yaani utaona kuna vitu vinapungua kidogo kidogo.utaona mawasiliano yanapungua,utaona hakujali,utaona hana muda na wewe.usisubirie akuambie kabisa hakutaki.na ili usiumie sana jifunze kumuacha aende.ukiachwa jifunze kusema japo nimeanguka ntasimama tena.ila jifunze kumsoma mtu ambaye anadai anakupenda wakati hakupendi.

Iko hivi maumivu ya mapenzi ni magumu lakini niamini mimi.kabla hatujaweza kutembea lazima tuanguke mara moja au mara mbili na saa zingine utasimamia meza.sasa mdau wetu mzuri naamini kabisa kuwa kakuacha lakini ndo unajifunza kutembea.ipo siku utapata mtu sahihi.unachohitaji usikate tamaa....
.. Nani kanielewa zaidi leo...

MUNGU AKUPE MACHO

Chapisha Maoni

0 Maoni