BROTHERS

Image result for lovers african couple photo style

1.Mkeo anabadili jina lake kwasababu yako.

2. Anahama nyumbani kwao kwasababu yako.

3. Anaacha familia yake kwasababu yako na kuondoka na wewe.

4. Mkeo anajenga nyumba na wewe.

5. Anabeba ujauzito wako.

6. Ujauzito wako unabadili umbo lake na kuwa mnene.

7. Anateseka chumba cha uzazi kwa maumivu makali kwa ajili ya mtoto wako.

8. Na mtoto akizaliwa anasubiri umpe jina unalolipenda wewe.

Mpaka kifo chake atakufanyia kila kitu, kukupikia, kusafisha nyumba yako, kuwatunza wazazi wako, kulea watoto, kubana matumizi ili msevu pesa, kukushauri, kuhakikisha unapumzika, kujenga mahusiano mazuri ya familia. Wakati mwingine anaweza hatarisha afya yake, uhai wake kwa ajili yako. Anakufumania analia kisha anakusamehe.

Brother, muheshimu mwanamke katika maisha yako, sababu kuwa mwanamke si jambo rahisi. Mfanye Mke wako kuwa kiumbe mwenye furaha pindi unapokuwa nae maana muda wa furaha kwake ni mdogo sana kuliko anavyokuridhisha wewe.

Chapisha Maoni

0 Maoni