MWANAMKE ULIYEOLEWA

Image result for lovers african couple photo style

Fanya siku moja umwangalie mumeo usoni akiwa amelala, halafu kaa na utafakari, jiulize maswali???
Huyu ndie mume wangu aliyenifanya niwaache wazazi wangu kwa ajili yake.

Sina uhusiano naye wa damu ila amekuwa mshirika wangu, mpenzi wangu, faraja yangu kuliko ndugu wa damu kwa sababu tunachanganya pamoja kila kitu sio damu tu.
-kwanini nisimpende
-kwanini nisimthamini
-kwanini nisimjali
-kwanini nisimsikilize
-kwanini nisiwe chini yake
-kwanini nisimfunilie moyo wangu?

Mumeo ni mtu muhimu sana katika maisha yako hata ukifanya dhambi mola ataenda kumuuliza na yeye pia,je ulimtumia vipi msaidizi wako niliyekupa?
Ulifunguaje moyo wake ili uone thamani ya kile alichobeba kwa ajili yako?

Siku moja akirudi kutoka kazini mkumbatie kwa hubba mshike mkono wake na uubusu, huo ndio mkono unaohangaika kufanya kazi ili muishi, mle chakula mshibe, mvae mpendeze, msiadhirike mbele za watu katika jamii.

Amekuwa sehemu ya maisha yako, amekuwa kama pande la nyama katika mwili wako, mara nyengine anawanyima ndugu zake wa damu ili akupe wewe. Huyo ndiye mumeo ambaye Mwenyezi Mungu amemsimulia kwamba siku utakapokufa akiwa radhi na wewe basi unaenda peponi moja kwa moja.

Yaani imeandikwa mke ataokolewa kupitia Mumewe na aliumbwa kwa ajili yake ila mume aliumbwa kwa ajili ya Mungu.
KUMBUKA: UKIMKOPESHA MAHABA ATAKULIPA MAWADDA

Chapisha Maoni

0 Maoni