
Kama unataka kuwa na amani katika maisha yako acha kuangalia alitembea na nani na angalia anatembea na nani sasa. Kuna watu ambao wanajitafutia magonjwa ya moyo, una mpenzi wako anakupenda na anaonyesha kuwa anakupenda, hajawahi kukusaliti na haonyeshi hata dalili za kukusaliti, lakini kwakua unajua alitembea na nani kila siku nikuulizia kuhusu huyo mtu, kila siku unakua na wasiwasi ukimuona huyo mwanamke au mwanaume aliyewahi kutembea naye.
Unajilinganisha kwa kila kitu na kutaka kuwa bora zaidi ya hao wanaume au wanawake zake. Katika maisha unatakiwa kujua kitu kimoja nilazima kuna mtu atakuzidi kitu flani lakini kumbuka kuwa huyo ambaye unaona kama kakuzidi na wewe kuna kitu ambacho umemzidi, unaweza usikione au ukakiona kidogo lakini ndiyo hivyo umemzidi na inawezekana hata yeye anatamani kuwa kama wewe.
Lakini pia kumbuka huyo tayari anaitwa “Mpenzi wa zamani” kuna sababu waliachana, kuna sababu walishindwana ndiyo maana uko naye wewe sasa hujitendei haki kujilinganisha naye na kama ukitaka kuwa kama huyo wake wa zamani basi jua kua mtaachana kama walivyo achana wao. Hivyo hembu acha kujiumiza kichwa na watu amabo hawanathamani katika maisha yenu ya sasa, kama alikua wazamani kwanini akunyime furaha sasa.
0 Maoni