HATA KAMA KAKUPENDEA PESA MUONYESHE MAPENZI KWANI BILA MAPENZI AKIZIZOEA PESA ATAKUSALITI!



Image may contain: 1 person, standing

Wanaume wengi wenye hela au mwanaume ambaye alikua hana hela na kuzipata katikati ya ndoa au mahusianao huamini kwamba kila mwanamke anapenda pesa, kwamba ukiwa na pesa basi unaweza kumfanyia mwanamke kitu chochote kile na yeye akavumilia kwakua wanawake wanapenda pesa. Nikweli kama wanadamu wengine wanawake nao hupenda pesa, pesa hurahisisha mambo mengi sana.
Lakini kitu kimoja ambacho wanaume wa namna hii husahau nikua pamoja na kupenda kwao pesa huko lakini pesa huzoeleka. Pesa ni kama chakula kizuri, mtu hukipenda kula mwanzoni na kutamani kukila kila siku, lakini baada ya muda kama mtu hatachanganya na chakula kingine basi hukinahi na kutokutamani tena kukila.
Hii ndiyo maaana wanaume wengi wenye pesa au wale ambao hawana pesa wanavijihela lakini wanaamini wana pesa na wamependewa kwasababu ya pesa husalitiwa na hata kuachwa. Iko hivi mwanzoni kweli mwanamke atafurahia pesa zako, atavumilia uzinzi wako na dharau zako, atavumilia kutokufika kileleni kwani kila mara akiwaza kuondoka hukumbuka kua una pesa na kama akiondoka basi atazikosa.
Lakini baada ya muda huzizoea zile pesa, si zipo, anazoea kuendesha gari zuri, kuvaa vizuri, kula vizuri na kufanya chochote kile ambacho kinahitaji pesa. Sasa pesa haimpi tena furaha, bali atataka vitu vingine, wakati wanawake wenzake wakimuonea wivu kwakua ana mwanaume mwenye pesa yeye atakua anawaonea wivu kwakua waume zao wanajali, wanaongozana nao, wanawapigia simu, wanawadekeza.
Atawaonea wivu namna ambavyo wanahangaika wakiumwa, kusikilizwa na yeye kutamani kufanyiwa hivyo. Kwamba katika maisha tunatamani vitu ambavyo hatuna na si vile ambavyo tunavyo, sasa wewe ushampa pesa anazo, hawezi kula Kuku mia au kupanda magari mawili hivyo atahitaji kitu ambacho hana na ni mapenzi hivyo usijishaue tu nina hela hawezi niacha, siku akizikinahi hizo hela atakuacha kwani atatafuta kitu cha ziada, badilika kua Mwanaume.

Chapisha Maoni

0 Maoni