UNAPOLALAMIKA KUWA MPENZI WAKO ANAKUSALITI MTENGENEZE KWANZA AWE WAKO TU

Image may contain: 1 person, standing and outdoor


Unapolalamika kuwa mpenzi wako anakusaliti hakikisha kuwa umemfanya kuwa mpenzi wako kwanza. Kama uko kwenye mahusiano na mtu lakini unaweza kukaa wiki au mwezi humtafuti, simu zote akupigie yeye na kila mkitaka kuongea unajifanya uko bize, anakutumia meseji gazeti unajibu ‘ok’ anakupigia kukujulia hali hata huchangamki ni ‘mhhh… sawa…usiku mwema”

Akiwa na shida hata kama si ya kifedha huwezi msikiliza na kumpa pole. Kila saa uko bize na wanawake wengine au wanaume wengine hata kama hutembei nao, halafu unasema kuwa ni mpenzi wako! Yuko na wewe lakini hajui kama nyie ni wapenzi au wajenzi! Unafikiri yeye ni mjinga akae kusubiri mizimu ya ukoo wenu ikuambie sasa mjali mpenzi wako! Hapana ni lazima atafute namna nyingine ili hata ukimwaga halii sana!

Unapokua na mpenzi wako mfanye ajione mpenzi wako, kiasi kwmaba hata akikusaliti siku moja aseme “Pale kweli nilichemsha, yule fala alikua ananipenda!” lakini unajifanya kuwa wewe ndiyo wewe, yaani ni kama hawezi kupata mtu mwingine zaidi yako! Acha ufala, kuna weni tu zaidi yako wanamtamani na wewe wala huna kitu cha maana au kipya ambacho sisi wengine hatuna ndiyo useme eti hawezi kuishi bila mimi!

Kuna watu wanajifanyaga kwamba wao ndiyo wao, wakishapendwa wanajiona kama ni ‘Oxygen’ kwamba mtu huwezi kuishi bila wao, lakini ukiwaangalia watu wenyewe ni ‘Makande’ tu tena ya maharage mabichi ukila sana yanakuongezea mashuzi tu na kukuharibia siku yako! Ukishamuacha sasa ndiyo anarudi na kujifanya sijui nimeumizwa, umenipotezea muda wangu, nakupenda, nilikua na mipango mingi sijui na nini nini? Kama unampenda muonyeshe kuwa unampenda hakuna upendo wa ndani ndani!

Chapisha Maoni

0 Maoni