
SHIDA MOJA YA WANAWAKE NIKUWA katika mahusiano wanapenda hivyo hivyo, wanamchukulia mwanaume jinsi alivyo na kumpenda hivyo hivyo, wengi wnawaza ‘kikubwa ndoa’ mwanaumea alikua ni mzinzi, alikua anakupiga, alikua ana kisirani, alikua ana kila aina ya uchafu lakini kwakua ulishakaa kwenu sana unaona bora niolewe.
Ukiingia kwenye ndoa sasa ndiyo unadhani ameshakua wako, yaani wanawake mnakaa mnadhani kuwa labda mwanaume ni kama Simu ya mkononi, kwamba ikiwa dukani huwezi kuifanya chochote, lakini ukishainunua unaweza kuifanya chochote unachoitaka, uamue kuizima, uamue kudownload Instagram au chochote kile.
Umeingia kwenye ndoa kuna rafiku ulimkuta nao unataka aachene nao, ulimkuta jamaa mlevi eti unataaka aache pombe kisa eti kakuoa, kwani wakati unamkubali si kuna kibao ambao walikua hawanywi pombe, alikua ni Malaya, alitembea mpaka na ndugu zako leo kaingia ndani eti unataka aache umalaya!
Ishu iko hivi, ndoa haibadilishi tabia za mwanaume, ndoa inabadilisha tu hadhi kutoka msela kuja mume wa mtu, lakini kama alikua mlevi basi atabaki na ulevi wake, kama alikua ni Malaya basi atabaki na umalaya wake. Unapoamua kuingia kwenye ndoa na mtu ingia kwenye ndoa ukijua kuwa huyu ni mtu wa namna flani!
Angalia tabia zake na jifunze namna ya kuishi kwenye ndoa na hizo tabia na si kutumia muda wako mwingi kujaribu kumbadilisha. Kwanza hatabadilika, utaishia kuchanganyikiwa tu, lakini pili atakuchoka, kwakua wewe ndiyo umebadilika, yaani wakati mko kwenye uchumba ulikua unmfumania unamuomba msamaha, leo kakuoa unamfumania unapiga kelee nani anataka hivyo vitu!
Utaishia kuachwa na kusema wanaume wopte ni mbwa wakati tatizo ni wewe. Kuna wahaume wanabadilika kweli lakini ukiongea na wanawake wengi utakuta kua, wanaume wao alikua na visirani na tabia hizo hizo kabla ya ndoa ila walikubali kuolewa kwa imani kuwa wanaweza kuwabadilisha, dada utakufa na kisirani bure, mwanaume anabadilika akiamua na habadilishwi kwa kelele.
0 Maoni