Sijaelewa ni mantiki gani iliyotumika kwenye kuidhinisha raia kujipima mwenyewe virusi vya Ukimwi.Kwa uelewa wangu mdogo,sifahamu kuhusu wengine ambao pengine wanaupeo mpana na wanaangalia mbali kuliko mimi,kitendo cha kujipima ukimwi kinaambatana na hofu na psychological disturbance ya kutosha kutokana na ugonjwa wenyewe ulivyo tishio.Hata kama hujawahi kufanya tangu uzaliwe,hata kama hujawahi kuongezewa damu kwenye hospitali yoyote ile au kuwahi kujikita kwenye mazingira yoyote yanayoweza kukufanya uambukizwe na ugonjwa huu.Ukiskia kupima lazima macho yakutoke!Mapigo ya moyo lazima yakuende kasi tena kasi kwelikweli.Hiyo ni kwa ambaye anajifahamu hajawahi kufanya wala ku "interact" na mazingira ya kumfanya aambukizwe.
Kwa wale wa upande wa pili sasa!Wazee wa chomeka chomoa,bandika bandua!Leo huyu kesho yule,hawa ndio hatari fire!.Kumshawishi kwenda kupima sio kazi rahisi,ni kazi ngumu sana kama ilivyongumu kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano.Hata akifanikiwa kufika hospitalini kwenda,huwa hatulii!Mguu nje,mguu ndani.Mshauri nasaha akianza ule ushauri wake ndo kabisaaa,jamaa anajiona kama vile wanamsema yeye,picha lukuki za mazishi yake zitamjia kichwani.Yaani anajiona tayari amesha athirika na ushauri wote wa daktari anaona kama una mlenga yeye kumbe sivyo!.Daktari akifikia kipengelea cha "KUPATA UKIMWI SIO MWISHO WA MAISHA,ZINGATIA CHAKULA BORA,KUMEZA VIDONGE VYA
ARVs KILA SIKU,ZINGATIA MAZOEZI nk"..Basi jamaa nguvu zinamrejea kwa kasi,anajiapiza kufuata kila ushauri ili aziongeze siku za kuishi duniani.Shughuli inaanza pale anapoambiwa karibu kwenye chumba cha vipimo,macho yanamtoka kama mjusi!anasahau ushauri wote,hofu na woga unaanza upya!Harufu ya kifo anaiona mbele yake,mshauri nasaha ataanza upya kumtongoza jamaa akubali kupimwa kwa maneno yao yalee "KUTOKUJUA KAMA UMEATHIRIKA NI KUJICHIMBIA KABURI MWENYEWE,BORA UJUE UMEATHIRIKA ILI UFUATE MASHARTI NA UISHI MUDA MREFU",jamaa anatongozeka.Akiingia,baada ya vipimo kuchukuliwa anapotea mazima na majibu anayatelekeza!.Anaona kujuwa kuwa ameathirika ni kujiua kwa stress,ni chanzo cha kutengwa,japo haisaidii chochote maana kama umeathirika umeathirika tu,hakuna kinachobadilika.Hapo ndipo umuhimu wa mshauri nasaha inaonekana tena,kuhakikisha anaongeza ushawishi wake ili muhusika afuate majibu yake kwa kumuhakikishia usiri na akimpatia majibu yake basi anatoa ushauri ulio bora ili mteja wake huyo asichukue maamuzi magumu ya kujiua kama ameathirika,kama hajaathirika basi atampatia misingi na kanuni bora za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu hatari!.

Haya sasa,wenzangu na mimi tujipime wenyewe si balaa hilo!.Tena unajipima ukiwa mafichoni kulee jikoni umebana na mlango ili wanazengo wasikuone.Unasahau kuwa jikoni kuna silaha za kutosha,mwiko uko pembeni😀,uma yenye misumali minne kwa mbele iko pembeni inayasusubili majibu yako kwa hamu😀,kisu cha kukatia nyanya na nyama zilizochinjwa na wagogo kiko kwa pembeni kinakucheka kwa huruma.Huku ukitetemeka,jasho limekutoka mithili ya mama anayesonga ugali wa watu kumi kwa jiko la mkaa.Unajitahidi hivyo hivyo mpaka unafanikiwa kujipima,badala ya kuangalia kifaa kilichotumika kuipima damu yako ili uone majibu kama umeathirika au laah!Wewe unaangalia pembeni hutaki kuwa shahidi wa kitakachotokea...!Mshauri nasaha hayupo,mlango umebana,jikoni silaha za kutosha,ugonjwa wenyewe unaojipima Ukimwi!Haya kazi kwenu....
0 Maoni