
Mwanaume anakutongoza, anakudanganya kuwa anakupenda, unamkubalia aakuja kindoa ndoa kabisa. Mwisho unakuja kugundua kuwa kumbe ana mke wake, au si mke lakini ana mwanamke, anaishi naye, na wamezaa nay watoto.
Anakiri kweli ana mke, anakuambia kuwa kabisa siwezi kumuacha lakini bila aibu anakuambia kuwa anakupenda, anatamani kuendelea kuwa na wewe kama mchepuko au mwanamke wake tu lakini hamuachi mke wake.
Mwingine anakuambia kuwa ni kweli, anaanza kukuelezea matatiozo ya huyo mke au mwanamke wake wanayeishi naye kisha anakuambia kuwa nitamuacha taratibu. Mwanaume wa namna hiyo basini mshenzi.
(1) Kwanza alikudanganya, inamaana alikua tayari kukuharibia maisha yako wewe, umtambulishe kwa ndugu, ubebe mimba yake na ukatae wanaume wengine kusema una mtu kumbe mume wa mtu, huyo si mshenzi ni nini ana mke au anaishi na mwanamke si mpenzi tu wa kuacha kesho!
(2) Anakuambia kuwa atamuacha huyo mwanamke mwingine taratibu. Inamaana anamharibia mwanamke mwingine maisha, kwamba kama ni kweli basi anaishi naye anazidi tu kumzalisha huku ana mpango wa kumuacha, huyo si mshehzi ni nini?
Dada yangu najua inauma, kakuumiza, najua una hamu ya ndoa inawezekana ushakata na tamaa na unajiona una mikosi ila huyo mtu hakufai. Kudanganywa ni kawaida, hata wanaume wanadanganywa lakini kujidanganya kuwa atamuacha mke wake kwaajili yako basi kama unamsoma Iddi Makengo na unajidanganya hivyo basi nikupe tu pole!
*Muangalie usoni na muambie tu kuwa wewe ni Mshenzi*
0 Maoni