
Kuna tofauti kati ya wanawake na wanaume wakati wa kuchepuka, mwanaume hata kama anachepuka na mke wa mtu anajijua kuwa anachepuka na mke wa mtu, yaani piga ua hawezi kuvuka mipaka ukakuta anachukua simu, anampigia mume wa mchepuko wake na kumuambia kuwa mimi ni mume mwenzako nilikua nakuambia tuko wawili! Hakuna kiru kama hicho wanaume wanajua nafasi zao.
Lakini sasa dada zangu, yaani wakishaanza kuchepuka, wakahisi wanapendwa, kwakua mwanaume kila siku akija kwako anakuambia matatizo ya mke wake, yaani kila akija kwako anakuambia mke wangu hivyo, mke wangu vile, mke wangu angekua kama wewe, mke wangu sijui nini na nini basi mnaamini kabisa kuwa ni kweli!
Mnaanza kuwashwa, mnaanza kujiona nyie wa maana zaidi, mnatamani kujulikana, unachukua simu unampigia mke wake, eti unamuambia nilikua nakuambia tu kuwa tuko wawili ukae ukijua kuwa hauko peke yako! Yaani wanafikiri ukishamuambia mke wake hivyo ndiyo ataondoka na kuiacha ndoa ili aolewe yeye, au ndiyo mwanamke atakua na kisirani mpaka nini!
Kwanza inawezekana mko kumi, lakini huyo mwanamke hakimbiio ndoa, inawezekana alikua anamjua mume wake Malaya tangu siku ya kwanza anamchumbia, unajitutumua kuongea. Dada mko wawili kweli, lakini unatakiwa kujua kuwa gauni na tambala la deki hizo zote ni nguo mbili ila moja inavaliwa na nyingine inafutiwa miguu inaishia mlangoni!
Wewe kusema mko wawili haimfanyi akuoe, mwanaume anayekupenda anamuacha mke wake anakuoa, au anakufanya mke kiasi kwamba huna haja ya kumpigia mke wake kujitangaza. Ukiona kuwa unafikia hatua ya kumpigia simu mke wake basi jua kuwa hata wewe huna furaha, nyumba iliyopikwa pilau haiweki bango kusema tumepika pilau abli harufu tu linatangaza.
0 Maoni