HAKUNA MWANAUME ANABADILIKA KISA MWANAMKE ANALALAMIKA

Image may contain: 1 person, smiling

Hakuna mwanaume ambaye anabadilika kwa mwanamke kulalamika, yaani kama kungekua na mwanaume anabadilika kwakua mke wake analalamika basi ndoa zote zingengekua na amani raha mstarehe kwani wanawake wengi wanajua kulalamika, lakini wanaume washazoea na wanajua kabisa kuwa nikifanya hivi basi atalalamika.

Kulalamika sana na kununa sana kunafanikisha mambo mawili tu katika mahusiano au ndoa;

(1) Kuondoa amani ndani ya nyumba na kumfanya mwanaume kuikwepa nyumba zaidi, kumsukuma mbali ili kukwepa kelele na hata kumuacha mwanamke kabisa.

(2) Mwanamke mwenye kisirani, ambaye hana raha na anayechukiwa na kila mtu, kwanza mume kwasababu ya kelele, pili ndugu kwasababu ya kuwalalamikia kila siku na tatu watoto kwakua kila dakika umenuna na mara nyingi unawashushia hasira wao.

Wanaume hawaogopi kulalamikiwa wala kununa kwa mwanamke kwasababu moja tu, mwanaume anajua kuwa kama mke wako bado anakulalamikia na kukununia basi bado anakupenda. Lakini wanaume wote wanaogopa wanawake wenye furaha zao.

Ndiyo maana hataki ufanye kazi kwani anahisi itakupa furaha, hataki hiki hataki kile. Mwanaume anayekupenda atakuheshimu pale utakapojipenda na kuacha kuumizwa na dharau zake kisha ukadili na maisha yako, una furaha yako. Kwanza atahisi una mwanaume mwingine unechepuka ndiyo anakupa furaha, atakufuatilia weee mpaka atachoka.

Chapisha Maoni

0 Maoni