
Ukisilia mtu analalamika kuwa nimempigia mpenzi wangu simu mara tano hapokei? Nimemtumia meseji zaidi ya kumi hajibu basi jua kuwa huyo anayelalamika ndiyo mwenye matatizo! Narudia, ukisikia mtu analalamika hivyo jua kuwa huyo mtu ndiyo mwenye matatizo. Hivi nimekupigia simu ya kwanza, yapili, ya tatu hupokei kwanini nipige ya nne?
Hata kama umelala mbinguni kuna mambo ulikua unashughulikia na malaika si ukirudi utakuta misss call na ukinihitaji unanitafuta? Lakini nakutumia meseji mbili hujajibu kwanini nitume ya tatu! Kana kwamba hiyo yatatu nimeandika na wino wa makaburini utashtuka na kunipigia!
Najua mpo wengi ila mpenzi wako akishaona unamnyenyekea kana kwamba yeye ndiyo anagawa maandazi motoni basi atakusumbua na kukuchafua moyo mpaka hutatamani tena mapenzi. Inatokea hivi kwa watu ambao hawajipendi, wale watu ambao wanaamini kuwa mapenzi ni kila kitu!
Hawa ndiyo wanasumbuka kila siku lakini ndiyo wanaumia kila siku. Ndugu yangu huyo mtu ana namba yako, kama anakutaka atakupigia na kama hakutaki akaogee mbele kwani yuko peke yake, najua labda ulipata shida kumpigia lakini kama unampigia simu mtu mara tano na hapokei na bado unaendelea kupiga basi wewe ni msumbufu, hayo si mapenzi tena ni ahdabu.
Ni kama nuna maisha, huna furaha yako hivyo unatafuta wengine kukufurahisha bila kujua kuwa unawaharibia siku zao! Badilika na jifunze kusema kuwa kama nimepiga mara mbili, nimetuma meseji mbili hanijibu sitamtafuta mpaka anitafute, ujiseeme kabisa akikaa kimya simtafuti kama vipi labda mkiwa motoni mkitafuta connection za maji!
Jifunze kunipenda, najua ni ngumu ila kuliko kumuwaza huyo mtu hembu mwaga maji ndani kisha jipe kazi ya kuwaza namna ya kuyatoa, utamsahau!
0 Maoni