UNAPOAMUA KUFANYA KITU CHA MAENDELEO NA MPENZI WAKO BASI HAKIKISHA UNAZINGATIA MAMBO HAYA MAWILI!

Image may contain: 3 people, people smiling, people standing

Kama unafungu biashara na mpenzi wako, mwanaume/mwanamke ambaye bado hamjafunga ndoa na kutambulika kisharia basi hakikisha unazingatia haya mambo mawili, inaweza kuwa ni baishara, kiwanja, shamba maduka na kitu chochote kile. Lakini kama ni uwekezaji wa mud amrefu, kitu chochote mnanunua ambacho unajua kua mkiachana utaumia basi usikifanye kama huna uhakika na mambo haya. Achana na upuuzi kua mnapendana hawezi kunitrapeli, kumbuka watu wote waliotapeliwa walikua wanaaminiana.
(1) Jina lako linakua kwenye naraka zote; Hiki kitu mara nyingi kinawakumba wanawake, anataka kufungua biashara na mwanaume jina linatumia la mwanaume, wanataka kujenga wanajenga katika kiwanja cha mwanaume, ni nadara sana kuona mwanaume anajenga katika kiwanja ambacho kina jina la mwanamke tu. Ingaw amimi siafiki hata kujenga na mpenzi wako kwani hakuna uhakika kama mtakuja kuoana lakinia ngalau hakikisha kua kiwanja, leseni ya biashara, kadi ya gari na chochote kile kina jina lako.
Mara nyingi wanaume wakitaka kuwatapeli wanawake kuna msemo wanautumia “Inamaana huniamini unaona kua nitakutapeli, kama hunaimini kitu kidogo kama hiki tukioana itakuaje!” Dada kama yeye hakuamini mpaka kuweka jina lako, tena sio lakwako peke yako, hapana majina yenu wawili wewe unamuamini vipi? Lakini kumbuka labda alikua na X wake waliachana wewe una nini cha ajabua sikuache, kua makini watu wanatapeliwa na Mama zao sembuse huyo umemkuta ukubwani!
(2) Unahusika moja kwa moja katika uendeshaji; Hii pia hutokea mara nyingi kwa wanawake, kwanza mwanaume anakuambia tufungue biashara flani, wewe ulikua huna hata wazo la biashara, hata hujui biashara wala nini, au unamkuta alikua anafanya biashara flani anakuambia umuongezee mtaji, anafungua biashara lakini kila kitu anasimamia yeye, yaani hataki hata ujue mahesabu na ukiuliza sana utasikia”Inamaana huniamini!”
Lakini inawezekana hata hakuzuii, ni wewe tu na ufalafala wako uanajisemesha “Mimi mambo ya magari, biashara sijui!” acha huo ujinga, ukiona mmefungua biahsara, hata kama ina jina lako, mmenunua kityu labda mashamba au kiwanja na hakishirikishi katika uendeshaji au wewe hushirik basi jua kua uankaribia kauchwa na karibuni utapigwa. Kama umependa kiasi hicho mpaka kufanya kosa la kufungua biashara na mpenzi wako basi hakikisha kua unaweza kufuatrilia kila hatua na kujua uendeshaji wake.

Chapisha Maoni

0 Maoni