
Leo naomba niongee kidogo na hawa mawifi, nyie wanawake ambao kila siku mnacomment na kulalamika mnanyanyaswa kwani nyie ndio hao hap mawifi. Una miaka 25 hujaolewa huna kazi unaenda kwa Kaka yako. Unajiambia kabisa “Ngoja niende kwa Kaka yangu nikapumzike!”
Umeolewa huko ndoa imekushinda, umemsoma Iddi Makengo umeamua kukimbia vipigo, badala ya uende kutafuta maisha unasema “Ngoja niende kwa Kaka yangu nikapumzike!” Kaka yako kaoa, ana mke wake, anampenda, walikua wanaishi kwa raha mstarehe lakini ukishakuja tu unakuja na visirani vyako.
Unajikuta unanuna tu bila sababu, kwanza unaanza kudhani kwakua Kaka yako umezaliwa naye tumbo moja eti una undugu naye, una haki naye, wewe ndiyo wamaana zaidi kwake na wewe ndiyo kila kitu. Unaanza kupanga mashariti, mara sitaki hiki, mara watotop walelewe hivi mara hivi mara vile!
Taratibu wifi ambaye mwanzo ulikua unamuelezea matatizo yako au wakati unasoma anakujali jali na vi manukato na vihereni unaanza kumuona kichomi na yeye anaanza kukuchoka. Umefadhiliwa badala ushukuru na ujiongeze kuwa nimesitiriwa hapa nikae miezi miwili na mimi nikadange kivyangu wewe umeng’ang’ania kwa Kaka yako utafikiri unataka akuoe mke wapili!
Kaka yako hana uhuru, dada yake ushazoea kutwa kucha jikoni unapita na Kanga moja kifuani nyinine kiunoni, yaani unazunguka tu kwa kaka yako na msidiria ambao una wiki haujafuliwa kwanza ushatatuka kisa tu kwa Kaka yako! Eti maisha yamekushinda sijui ndoa imekushinda unakuja kupumzika!
Yaani ulivyo na roho mbaya ushaanza kumuwazia na Kaka yako kifo, eti Kaka akifa wifi atachukua mali zote! Aisee ondoka hapo kwa Kaka yako, watu wanataka kutengeneza watoto kwa raha wewe unang’angania, kaka yako anashindwa hata kumtoa mke wake out kias umemng’ang’ania, ushakua mkubwa ondoka, amekufadhili mwezi mwisho miezi mitatu baada ya hapo tafuta kwako!
0 Maoni