MY DIA JIULIZE

Ulikua unafanya nini kabla ya kukutana naye? Hili ni swali ambalo unapa swa kujiuliza. Kabla ya kukutana na huyo mwanaume nina uhakika ulikua na maisha yako, hata kama hayakua mazuri kihivyo lakini alikuona na hayo maisha na akakupenda nayo.

Sasa umampata mwanaume badala ya kuishi maisha yako unataka uishi yake, hapo hajakuoa na wala hata uhusiamno wenu haujawa imara. Wanawake wengi wanapokua na wanaume wanaowapenda, wanaoona labda nao wanawapenda huanza kujisahau.

Wanasahu kutengeneza maisha yao kabisa na kusubiri wanaume, hapa kuna namna mbili. Namna ya kwanza ni katika kujipa furaha na namna ya pili ni katika kujitegemea kiuchumi. Tuanze na jambo la kwanza, kujipa furaha, kabla yake ulikua unafanya nini?

Ulikua una marafiki unatoka nao kuburudika, ulikua unajinunulia zawadi, ulikua na hobi zako labda Muvie au TV na muziki, ulikua na vitu unapenda iwe ni kuvaa au kufanya. Lakini umempata kutwa kucha ni uko nayeye, unafanya kile nachotaka ufanye.



Related image
Ni boyfriend lakinia shakukataza kila kitu, lakini hajakukataza ila na wewe unaacha kufanya mambo ya kujifurahisha kila saa aunajikita kumfurahisha yeye. Unataka ukampikie,ukamfulie, ukamfanyie hiki. Usafiri naye akitaka na kila kitu anachaoitaka yeye. Kwa kifupi unasahau kuwa na wewe unatakiwa kuwa na maisha.

Hapa moja kwa moja unakua kama Kupe kumganda, unamnyima uhuru na anaona kama unamtegemea yeye kwa furaha yako, anaanza kukuchoka mapemaa kwakua ushakua Kupe mapema. Kwamba akiwa online ushatuma miemeseji eti lazima achat na wewe, kutwa unapiga simu kumi, kutoka unataka muongozane.

Asipokukumbuka kutwa nzima ushanuna, unaona kama hakujali si kwasababu hakujali bali kwakua wewe umeacha maisha yako na unataka kuishi maisha yake. Kwamba mwanzo si ulikua na ratiba zako, unafanya mambo yako kivyako lakini sasa unaangalia ratiba yake ndiyo ufanye mambo yako.

Sijui kama mnanipata lakini inakua kama vile unamsubiria yeye kwa kila kitu, unafanya mambo mengi sana anayotaka yeye kuasi kwamba huwi na maisha binafsi. Hata baadhi ya marafiki mliokua mnaongea na kubadilishana mawazo unakua huna muda nao kutwa kucha umegandana na mpenzi unaona ndiyo mahaba.

Chapisha Maoni

0 Maoni