KAMA MWANAUME HATAKI KUKUONYESHA ANAPOISHI BASI JUA WEWE NI MCHEPUKO !

Related image

Kama uko na mwanaume, ni mpenzi wako lakini hataki ujue anaishi wapi? Hata kama umekaa naye kwenye mahusiano kwa miaka kumi basi jua wewe ni mchepuko. Kuna mambo mawili hapo, inawezekana anaishi na mkewe au ana mchumba wake ambaye anamheshimu sana na hataki kukupeleka pale ukaja kumharibia.

Narudia kwakua nyinyi Dada zangu mnapenda kudanganywa kama mwanaume hataki ujue anapoishi basi jua kuwa huyo si mwanaume wako unatumika tu kingono. Hata kama anakuhudumia, anakujali na kukufanya kama Malaika kama hataki ujue anapoishi Dada yangu wewe ni mchepuko. Sasa wanaume kama hawa watakuambia naishi na wadogo zangu siwezi kupeleka mwanamke nyumbani.

Jibu ni rahisi akuonyeshe hata anapokaa kwa mbali tu, hata usiingile ndani. Lakini huo ni utetezi wa kijinga sana, tena mwingine atakuambia kuwa naishi na wazazi wangu siwezi kupeleka mwanamke.

Huo ni utetezi mwingine wakijinga, labda kama huyo mpenzi wako ni mwanafunzi wa chuo au ni kahaki elimu au hana kazi, huyo sawa nitamuelewa lakini kama ni mwanaume anafanya kazi anaweza kukupeleka ukapafahamu akakutambulisha kama mfanyakazi mwenzake. Au akasema alisoma nawewe na kakutana nawe mjini kama hataki kukutambulisha rasmi. Lakini pia anaweza kukuonyesha tu mimi naishi pale basi yakaisha.

Mwanaume kukupeleka kwa wazazi wake inaweza kuwa ishu wakati mwingine lakini kukupeleka kwake hapana. Hivyo muelewe akikuambia anaishi na wazazi wake muambie tu unataka kujua nyumba anayoishi na hao wazazi wake hutaki hata kufika. Ila kama anaishi mwenyewe na hajakupeleka kila siku anakuja kwako au kwakua wewe unaishi kwenu mambo yote mnaamalizia Gest Dada yangu acha kusubiri Ndege Bandarini.

Najua ushaanza kusema huyu hapana, najua kuna wanaume wanasema si kweli, lakini wote tunajua kuwa mwanaume unapenda mpenzi wako aje pale hata afue na kufanya usafi kidogo au apike. Hivyo asikupe sababu yoyote mtu anayeishi kwake, achana na hawa watoto wanaoishi kwao. Lakini kama yuko kwake hataki kukuonyesha, show zote mnafanyia kwako basi Dada yangu niwakati wa kutafuta vitambaa vya kufuta machozi pindi ukipewa kadi ya mualiko au ukisikia kuwa ameoa!
Imeisha hii

Chapisha Maoni

0 Maoni