Kuna wakati upweke unakufanya kuingia kwenye mahusiano ambayo sio sahih

Related image
Kuna wakati upweke unakufanya kuingia kwenye mahusiano ambayo sio sahihi, kuna wakati pia msongo wa mawazo unakufanya kumuamini mtu ambaye hukustahili kumuamini.

Ni wengi huingia kwenye mahusiano kwa ajili ya kupata Furaha, ni wengi pia huingia kwenye mahusiano kwa ajili ya kutafuta faraja. Unaonaje ukaitafuta furaha yako na faraja ukiwa mwenyewe? Kwanini usijipe raha mwenyewe? bila mtu inamaana huwezi kupumua?

Wewe mwenyewe tayari ushaumizwa vya kutosha kwenye mahusiano yaliyopita alafu unategemea tena kwenda kupata ahueni kwenye mahusiano mengine. Usipokua makini, huko unapoingia kuanzisha mahusiano ndio patakua pabaya zaidi. Hebu tulia kwanza jipe tathmini ya maisha yako, jaribu kufanya mambo mengine then mapenzi yatafuata

Chapisha Maoni

0 Maoni