Kila dada asome hii
My dia ufike wakati
Ujitambue sana na uwe zaidi
Ya kawaida..
Hebu nikwambie
Kama uliwahi kutoka kimapenzi na mwanaume mkaacha, kisha akarudi tena baada ya siku, wiki au miezi kadhaa akikuhitaji akalale na wewe siku hiyo hiyo, au siku ya pili au ya tatu mkatalie, mkatalie tena kwa herufi kubwa sana. Tena mfanye atambue wewe siyo wa aina hiyo, kwamba unaweza kutumika muda wowote anaotaka hata kama alipata bahati ya kukutumia hapo awali.
Kama kweli alikuwa ana mapenzi na wewe asingeenda kuhangaika na kutembea na wanawake wengine ikiwa bado anakuhitaji, mfanye ajue wewe sio wa kirahisi hivyo. Tena ikiwezekana mueleze misingi imara na mtazamo wako chanya kuhusu maisha ya kimahusiano. Kwa mwanaume mwenye nia ya dhati na wewe, ukishamueleza msimamo wako, lazima atavutiwa na wewe si tu kwa vile unajiheshimu, lakini ni kwavile unataka awe kwenye mstari sahihi ikiwa kweli anakuhitaji.
Jambo hili limekuwa wakikumbana nalo sana wanawake waliyowahi kuzaa na wanaume ambao hawakuwa na mpango wa kuwaoa, wamejikuta wakitumika tena kingono na wanaume hao hao hata licha ya kuwa tayari wapo ndani ya ndoa na wanaume wengine. Haiwezekani mwanaume alikukimbia tangu tu ulipomwambia wewe ni mjamzito hadi unajifungua hana habari, mtoto kazaliwa ndio anakuja kuhudumia, usikubali hakuhudumie na wewe kingono. Mruhusu amuhudumie mtoto wake ila usimruhusu akakutumia tena.
Lakini pia utakuta mwanamke mwengine anatumika kingono na mwanaume kwa kigezo cha mzazi mwenza wakati hata huyo mwanaume hana huduma yoyote kwa mtoto wala mama, huo ni ujuha.
My lovely sister, usijirahisishe kwa mwanaume kuendelea kukutumia anavyotaka hata kama amekuzalisha. Achana na mentality za hovyo kwamba “mtalaka hatongozwi” jipe viwango hata kama ilitokea bahati mbaya ulizaa nje ya ndoa. Kama ni wako Mungu amekuletea, atafanya kila liwezekanalo akuoe ila kama si wako, ujue kaja kukupotezea dira ya maisha yako.
Napenda wa dada mjitambue
0 Maoni