Mpedwa Ex…

Related image

Mpedwa Ex…

Nilishafuta namba yako. Nikafuta pia na picha zako, nikawachukia rafiki zako. Pumzi yangu ikawa yamoto kila lilipotajwa jina lako. 
Hivi ni tusi gani sijakutukana? Ni laana ipi sijakuombea kwa Maulana?

Vyote nimefanya na vyote bado havijanipa amani ninayoitaka. 
Sijui kwanini bado niko hivi mpaka leo. Sielewi. Ukweli sikupenda ujue kuwa unaendelea kuishi kwenye fikra zangu. Sikupenda kabisa uhisi kuna udhaifu ndani yangu.

I'm sorry. 
Kitu pekee nilichopenda kukufahamisha ni kuwa, sasa nataka nikuchukie.

Yes. Nataka nikuchukie.

Nataka nikuchukie mwa machozi yote niliyoyatoa kwa sababu yako. Nikuchukie kwa kumbukumbu zote ulizoziacha kwenye kichwa changu. Nikuchukie kwa alama za vidole ulizoziweka kwenye ngozi yangu. 
Kweli nataka nikuchukie.

Nataka nikuchukie kwa jeraha ulilolipanda ndani ya moyo wangu. Nikuchukie kwa muda nilioupoteza kwako. Nikuchukie kwa kukuamini, kukupenda, kukujali, kukuthamini na kukulinda.

Kweli nataka nikuchukie milele.

Nataka nikuchukie kwa jinsi ulivyonifanya nikaamini mimi si lolote bila wewe. Nikuchukie kwa ahadi zote ulizoziweka mbele yangu. Nikuchukie kwa namna nilivyoyaweka maisha yangu mikononi mwako.

Kweli nataka nikuchukie kwa kila pumzi yangu iliyosalia duniani. ;Nenda!!! Nenda!!!! Neeeenda... Wako Ex 
Yule uliyeapa huwezi kuishi bila yeye

Chapisha Maoni

0 Maoni