
Niseme kitu
Lengo la mahusiano sio kutembea mmeshikana mikono, ama kujipiga selfie pamoja ama kuvaa nguo za kufanana. Hayo mambo ni ya vijana wadogo. Hebu komaeni muwe na magari ya kufanana, hebu komaa mjenge nyumba nzuri, muwe na date nights, msafiri pamoja around the world. Na njia pekee ya kufanikiwa hayo ni kama wewe na mwenzi wako mtaamua kufanya kazi kwa bidii huku mkimtegemea Mungu. Tengenezeni hizo hela, Mpendeni MUNGU, Komaeni na Maisha Kimya kimya ili mng'ae hadharani. Yaani wewe na Mpenzi wako tu against the World. Oa ama olewa na mtu ambaye atatamani mjijenge zaidi. Ndoa ni moja ya njia ya kujijenga pamoja, kupeana muda wa kuwa na ndoto kubwa ya pamoja na kutimiza yale ambayo yalidhaniwa yanashindikana. Maisha ni mafupi mno kuishi na mtu ambaye anaridhika kimaisha mapema.💓💓💓😝😘😘✔✔
0 Maoni