
Dada
Acha kusifia wanaume wengine mbele ya mume/mpenzi wako, kama umemchagua huyo na unampenda au hata unamvumilia acha kusifia wanaume wengine hata kama si wapenzi wako, narudia hata kama unamsifia Kaka yako kwa namna ambavyo anamjali wifi yako jua hilo ni tatizo. Najua hufanyi kwa nia mbaya na wakati mwingine ni ili kumkumbusha mume wako majukumu yake lakini acha.
Kuna wanawake utawasikia, napenda jinsi Kaka yangu anavyoishi na wifi yangu, yaani wanavyotoka pamoja, wanavyofanya hiki na kile yale ndiyo mapenzi! Utasikia rafiki yangu na mume wake kama sijui nini, mwanaume anajua kujali, sijui Bosi wangu na mkewe hata kusifia watu kwenye TV sijui unasema flani ndiyo mwanaume anavyoishi na huyo mkewe.
Unapokua unaongea hivyo ni kama unamuambie mume wako kuwa yeye si mwanaume wa kutosha, unamuambia kuwa huridhiki na penzi lake lakini haiishii hapo ni kama unamuambia pamoja na kuwa huyo mwanaume unayemsifia huwezi kumpata lakini ukipata mwingine kama huyo basi uko tayari kwenda kwani huna furaha.
Narudia najua haikua nia yako lakini ndivyo ambavyo mumeo ataelewa. Sasa swali linakuja ufanyeje kama huridhikia na mambo anayokufanyia mumeo, kama unataka zaida. Jibu ni rahisi, muambie vile vitu unavyopenda akufanyie au onyesha furaha pale anapokufanyia hata kidogo tu. Kwa mfano badala ya kumuambia mume wako napenda flani anavyotoka na mume wake.
Badala ya kumuambia napenda jinsi Kaka yangu wanavyokula na wifi yangu, wanavyosikilizana muambie mume wangu napenda hata tuwe tunatoka pamoja mara moja moja au hata kumtoa wewe, muambie napenda tuwe tunakula pamoja au tenga chakula sahani moja mkae na mle pamoja. Ndiyo muambie unachokipenda kwake lakini si kumlinganisha na wanaume wengine!
0 Maoni