USIJILAUMU KWA JAMBO AMBALO HAUWEZI KUBADILI MATOKEO YAKE.


Image result for adrian mcdonald photography

USIJILAUMU KWA JAMBO AMBALO HAUWEZI KUBADILI MATOKEO YAKE.
Maisha ni safari ndefu,na katikati ya safari mwanadamu anafanya makosa mengi sana kupitia mawazo yake,meneno ya kinywa chake na hata matendo mabaya tunayowatendea wengine.
Ili maisha yawe na maana jambo la
kwanza ni lazima uwe na moyo wa kujisamehe mwenyewe,

Wengi wetu tumetumia muda mwingi kujihukumu,tunajilaumu sana kwa ajili ya mambo ambayo hayana suluhisho,
MFANO.....
#Unajilaumu kwa kupata mimba ukiwa form two ukashindwa kumaliza masomo,lakini umeshindwa kumshukuru Mungu kwa zawadi nzuri ya mtoto aliyekupatia,na bado una nafasi ya kurudi shule ukapata elimu sawa na waliokutangulia.
#Mwanaume unajilaumu kwa kuoa mke wa pili,wakati huo tayari umezaa naye watoto watano,ndugu yangu unachelewa kutafuta hela ya kuwahudumia,masna hiyo tayari ni familia yako na hao watoto hawataa kuja kuwa watoto wa jirani,
#Unajilaumu kwa kuzaa na mume wa mtu ambaye sasa hana mpango wa kuhudumia mtoto wake,Nakukumbusha tu maisha yamekua magumu sana kutegemea hela ya huyo ndugu,ulishafanya kosa la kwanza kwa kugumba macho na kuona huyo mume ni wenu wote,sasa usifanye kosa la pili la kushindwa kumpa mwanao mahitaji yako ya muhimu,Ila na nyie wanaume wa sample hii kwa ajili ya watoto hawa mtadaiwa
#Wako wanaojilaumu kwa kuwa kwa sababu ya shida za dunia hii waliamua kumuacha Mungu,wakawa walevi,wazinzi na wachawi kupindukia,Sasa leo wamegundua huko waliko hakuna faida wanashindwa kuendelea,my dia Mungu yule yule aliyemsamehe Daudi aliyezini na mke wa Uria,na bado akamwua Uria kuficha dhambi yake,Mungu yule yule bado anasamehe mpaka leo,Hujachelewa kumjia.
#Unajilaumu kwa ajili ya matusi makubwa uliyowahi kumtukana mwanadamu mwenzio,Ndugu yangu maneno yanasamehewa lakini hayasahauliki,
Ikiwa ulishawahi kuomba radhi,jisamehe na Songa mbele,

#JE WEWE UNAJILAUMU KWA LIPI???? Badilika leo,Amini Mungu amekusamehe,Jisamehe nawe moyo wako upate amani,songa mbele kwa ushujaa kukamilisha yanayohitaji juhudi zako ili ufanikiwe.Wewe sio wa kwanza kukosea chini ya jua na biblia iko wazi, "Tukusema hatuna dhambi twajidanganya sisi wenyewe na tunamfanya Mungu kuwa muongo"
Acha kujilaumu yajenge upya ok


Chapisha Maoni

0 Maoni