WEWE KAKA HUWEZI KUOA AU KUTEMBEA NA WAREMBO WOTE

ewe kaka
Related image

Huwezi kuoa au kutembea na warembo wote, wanawake wazuri siku zote wataendelea kuwepo, kila siku utakutana nao wapya. jifunze kuwa na adabu (self discpline) pamoja na kujidhibiti (self control). Chagua mmoja tu, mjenge awe wako, mfanye awe malikia wako! hii itakupunguzia gharama, itakutunzia muda wako, drama pamoja na magonjwa.

Vile vile hakuna medali, tuzo au nishani ya juu ya ushindi wa kuwa na wanawake wengi, bali ni kuzifungia baraka ambazo Mungu anataka kukupa na kujipeleka mwenyewe kaburini mapema. Jiongeze brother!

Busara yangu; A realman sees no other females becoz he only has eyes for his girl!

WANAWAKE wote ni wazuri, ni matunzo yako tu!! Ukimlisha mihogo kila siku lazima afanane na mihogo, lakini ukimlisha mboga saba lazima anone. Ukimvalisha madekio lazima afananane na madekio, lakini ukimvalisha nguo nzuri lazima akuvutie. Ukimpiga-piga ngumi kila mara lazima awe na manundu na makovu-makovu, lakini ukimdekeza lazima awe laini-laini...Utamu wa sigara ni kuivuta, siyo kuiwasha tu halafu unaitupa!! Baadhi ya WANAWAKE wanapenda kuamini kuwa WANAUME zao hawawezi kuwasaliti ati kwa sababu labda wao ni wapole, wazuri, wanayo shape, labda wanayo makalio makubwa na wanajali.
Hii sio kweli, wapo wanaume ambao wanawa-cheat wanawake zao wazuri zaidi ya Cleopatra Aisee, hivyo, kama Mwanaume wako hakusaliti, basi sio kwa sababu ya upekee wako bali ni kwa sababu ya AINA YA MWANAUME aliyochagua kuwa hivyo. Uaminifu wa Mwanaume hauhusiani kabisa na uzuri wa mwanamke, uaminifu wa Mwanaume ni yeye mwenyewe, uimara wake wa kukabiliana na vishawishi, kusimamia kiapo chake, aliye loyal na committed haswa..sio jambo la mchezo mchezo.

Chapisha Maoni

0 Maoni