
Kama umeoa na unamsikiliza Mama yako kwa kila kitu, kama umeoa na humshirikishi mke wako kwa kitu chochote, kama umeoa na ndugu zako wanaweza kumtukana mke wako au unajali matatizo ya ndugu zako kuliko mke wako, kama umeoa umemuambia mke wako hutaki afanye kazi lakini unahangaika kumtafutia mdogo wako wa kike kazi, kama umeoa kila kitu kinachotokea katika familia yako unawaambia ndugu zako, matatizo yote ya mke wako unawaambia ndugu zako.
Kama umeoa, ndugu zako wanapokulalamikia kuhusu mke wako wewe ni kumtandika makofi kumtukana na hata kujaribu kumfukuza basi ni suala la muda tu ile simulizi ya “House Girl Kiraka” inakuhusu. Nikuambie tu ndugu zako ni ndugu zako lakini hawana undugu na watoto wako, unamaana kwao kwakua sasa hivi una pesa na una wajali lakini ukifa leo au watoto wako wakikosa ada mtu wa kwanza kuhangaika ni mke wako.
Kama huniamini leo hembu wewe si una Baba yako mdogo/mkubwa, una Shangazi au mjombe. Hembu leo nenda kamuambia nina shida ya laki moja au kiasi chochote ambacho ana uwezo nacho. Fanya hivyo kwa miezi mitatu mfululizo halafu angalia kama atakupa, kisha jiulize je ingekua Mama yako angekusaidia au la? Nataka ujiuliza ukaribu ulionao wewe na Ndugu wa Baba yako mdogo/mkubwa au Shangazi kisha linganisha na ukaribu ulionao na Mama yako.
Jiulize kati ya Mama yako na Shangazi yako nani amehangaika sana na wewe ukiwa kwenye matatizo. Kama jibu ni Shangazi au Baba mdogo/mkubwa basi wapende ndugu zako kuliko mkeo kwani hao ndiyo watakua mababa wadogo/wakubwa na mashangazi wa wanao. Lakini kama jibu ni Mama yako basi mpenzi mkeo kwani yeye ndiyo Mama wa watoto wako na jinsi Mama yako anavyokupenda ndivyo ambavyo mkeo atawapenda wanao.
Hii sauti inatosha sana.
0 Maoni